SoC01 Waandishi wa habari wapewe kipaumbele katika kuibua maovu yaliyofichika, sambamba na kutoa elimu katika jamii

SoC01 Waandishi wa habari wapewe kipaumbele katika kuibua maovu yaliyofichika, sambamba na kutoa elimu katika jamii

Stories of Change - 2021 Competition

ItsMi

Member
Joined
Sep 13, 2021
Posts
66
Reaction score
31
Sekta ya habari ipewe kipaumbele Kwa kuwa ndiyo sauti ya jamii kwasababu kwa miaka mingi sasa imeendeleza jukumu lake la kuwasilisha taarifa mbalimbali kwa umma na katika kutoa elimu katika jamii katika kuhamasisha utekelezaji wa mambo mbalimbali yenye kuwaletea wanajamii hao maendeleo yao na taifa lao kiujumla wamekuwa wakihakikisha sauti na vilio vya wananchi zinawafikia viongozi ambao ndio waliopewa jukumu la kuwaongoza wanajamii katika hatua na juhudi za kulijenga taifa katika kuzingatia misingi bora ya kimaendeleo.

Pia Vyombo vya habari vinahamasisha shughuli za kimaendeleo na katika kuiweka jamii katika hali ya usawa na kuondoa machafuko mbalimbali kwa hamasa zao .pia wamekuwa wakitoa elimu mbalimbali na namna ya kujikinga na maradhi mbalimbali Ikiwa pamoja na kufichua maovu yaliyofichika
Pia kutoa hamasa kwa viongozi katika kutekeleza wajibu wao wa kuongoza na kusimamia raia na mali zao katika jamii
Na ndio sababu ya kwamba serikali inatakiwa iwape kipaombele wanahabari katika kuzungumzia yanayojiri katika kwa kuzingatia haki na usawa wa mtu mmoja mmoja Na taifa kwa ujumla wake.

hivyo wanahabari ni chachu ya maendeleo kwa jamii zetu hivyo wanayo haki ya kupewa uhuru wa kuongea bila vitisho vya namna yoyote na endapo watakuwa na haki ya kuongea tutaweza kudhibiti wahujumu uchumi na mali za taifa wenye kutumia uongozi wao vibaya katika kujinufaisha wao na familia zao.
vyombo hivi ni mahususi kabisa katika kupashana habari, Kuishauri jamii, Kukosoa viongozi wenye makosa mbalimbali, Na kutetea pasipo na haki bila upendeleo wa aina yoyote ile.
Waandishi wa habari wapewe haki ya kutoa habari kwa uhuru bila upendeleo kwa mtu au tasisi yoyote
Kwa pamoja kama taifa tutaweza kuunda mifumo imara ambamo itatusaidia kujua wapi ipo haki na wapi ipo dhuruma.
Kwa usaidizi mkubwa kutoka kwa waandishi wa habari ambao wamekuwa nasi bega kwa bega katika kufichua maovu na kuweka wazi njama zinazotumika na viongozi mbalimbali zenye kuleta dhuruma kwa jamii
Hivyo ni ombi letu kwa pamoja kwamba waandishi wa habari au sekta ya habari ipewe uhuru na ulinzi kwa sababu kazi yao ni kubwa ni mfano wa wawindaji wanaowinda wanyama wakali huku wakiwa mstari wa mbele kutetea haki za wanyonge
Asante

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Upvote 1
Back
Top Bottom