Waandishi wa habari wawili wa CPJ wanatuhumiwa kufanya kazi Tanzania bila kibali

Jay456watt

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2016
Posts
10,356
Reaction score
7,992

Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania imeelezea mazingira iliyowafanya waakilishi wawiili wa Kamati ya Kimataifa ya kuwalinda wanahabari CPJ, kukamatwa.
Msemaji wa idara hiyo Ally Mtanda amenukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema kuwa wafanyikazi hao walikiuka madhumuni ya ujio wao kama walivyoandika katika vibali walivyopewa wakati wakiingia nchini,kutokea Afrika Kusini.

Waakilishi hao wa CPJ walikamatwa na kuzuiliwa kwa muda kutokana na tuhuma za kufanya mkutano na waandishi wa habari, tofauti na madhumuni ya kufanya matembezi tu.

Bwana Mtanda hata hivyo amethibitisha kuwa, Muthoki Mumo na Angela Quintal, wamerudishiwa hati zao za usafiri.

Wawili hao pia wameruhusiwa kuendelea kuwepo nchini Tanzania kwa sababu bado vibali vyao vinawaruhusu kuendelea kuwa nchini humo hadi Januari 9 mwakani.

Awali Idara ya kimataifa wa uhusiano na ushirikiano nchini Afrika Kusini (DIRCO) ilisema waandishi hao wamerudi kwenye hoteli yao.

"Balozi wa Afrika Kusini Bw Thami Mseleku amekutana nao na kuzungumzia kile kilichotokea.

Kisha atazungumza na mamlaka za Tanzania. Msemaji wa DIRCO Bw Ndivhuwo Mabaya, alizungumza na Bi Quintal leo asubuhi," Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya Afrika Kusini ilisema kwenye mtandao wa Twitter.

Chama cha wahariri wa habari nchini Kenya kimelaani kukamatwa kwa waandishi hao wa habari na kutoa wito kwa serikali ya Tanzania kuwaruhusu kukamilisha kazi yao.

Maafisa waliojitambulisha kama wafanyakazi wa idara ya uhamiaji nchini Tanzania waliwakamata Quintal na Mumo kwenye hoteli yao mjini Dar es Salaam, kwa mujibu wa CPJ.

Maafisa hao walichukua bidhaa za wawili na hawakurudisha pasi zao za usafiri wakati waliombwa.

Quintal na Mumo kisha wakatolewa hotelini na kupelekwa eneo ambalo halikujulikana, Mara baada ya kukamatwa, ujumbe wa twitter ulitumwa kutoka akaunti ya Quintal, ukisema "Mungu ni mkuu tumeachiliwa na tunarudi hotelini," na kuzua hofu kuwa mtu fulani alitumia simu zake.

"Ujumbe wa @angelaquintal haukutumwa naye," aliandika mpwa wake Quintal, Genevieve Quintal, ambaye pia ni mwandishi wa habari. "Hii inaonyesha kuwa kuwa kuna mtu anatumia simu yake."

Akaunti za Twitter za Quintal na Mumo zimezimwa tangu wakati huo.
 
Balozi wa kenya alikuwa wapi? mbona kamuachia balozi wa SA apambane peke yake?
 
Hao kwanza walipaswa kupewa Bakora
Tanzania nunchi huru
ina sheria zakebwana
 
Huyo Mkenya pona yake kakamatwa akiwa na mzungu tena kaburu wa SA, hapo wabongo walibabaika na kuachia haraka bila ubishi, angekua na nyeusi mwenzake bado angenyea debe kwa miezi kadhaa au atokomezwe na wasiojulikana.
 
Huyo Mkenya pona yake kakamatwa akiwa na mzungu tena kaburu wa SA, hapo wabongo walibabaika na kuachia haraka bila ubishi, angekua na nyeusi mwenzake bado angenyea debe kwa miezi kadhaa au atokomezwe na wasiojulikana.
bora sisi tumewatia jambajamba..!!nyie hata ubavu wa kumkamata ngozi nyeupe hamna,viongozi wenu wanawaogopa sana wazungu!!
n:b:sisi hatujaanza leo toka enzi za nyerere mzungu akizingua tunamficha mahali pasipojulikana tunamminya weee akitoka anakuwa na adabu zote,unamkumbuka yule mzungu aliesema "ameiweka Tanzania yote mfukoni kwake"..au ulikuwa bado hujazaliwa weweeeee
 

Hehehe wapii, nyie juzi Makonda kakurupuka kwa kuanzisha ugomvi na mabwabwa, mumeguswa kidogo tu nyote mkanywea na kukubali yaishe, mawaziri kila mmoja anakimbilia kwa vyombo vya habari kutetea nchi isipokee kipodo. Nimesema siku zote maskini hana jeuri, unashikishwa ukuta maana hela za hao mabwabwa ndizo mnategemea aidha kwa misaada au wakija kama watalii.
Na ndio unaona mlipomkamata mzungu mwanahabari imebidi mumteme na kuachia kama kaa la moto.......hadi siku mtatoka kwenye lindi la umaskini ndio muzungumze, lakini kwa sasa mko mbali sana kuleee!!!
 
Munatuma vijasusi vyenu uchwara munategemea serikali isijue.
 
Wahindi kibao wanafanya kazi bila vibali!!

Hawa waandishi mlishawapeleka kusikojulikana
 
Wahindi kibao wanafanya kazi bila vibali!!

Hawa waandishi mlishawapeleka kusikojulikana
Si ukawaripoti hao waandishi wanaofanyakazi bila vibali kwenye mamlaka husika wachukuliwe hatua.
 
Hamna jipya, ni kawaida tu kwa nchi zinazotawaliwa na madikteta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…