Chujio
JF-Expert Member
- Jun 17, 2013
- 1,368
- 2,108
hili halijaanza jana wala juzi ila siku hizi imezidi mno na kuwa kero. tafadhali sana waandishi wa magazeti, naombeni mzigatie uandishi wa kiswahili fasaha na sahihi pasipo kukera wasomaji... unakuta mwandishi kabisa anaandika neno "razi" au "lazi" badala ya radhi kwenye gazeti linalosomwa na wengi.. au unakutana na lajisi, latiba kha! jamani, kiingereza tukosee basi hata kiswahili nacho? wahariri wa uandishi jamani angalieni hilo kabla ya kuchapisha habari rasmi, tunawasihi tu zingatieni matumizi na uandishi ulio sahihi wa lugha yetu, maana inaharibika kweli siku hizi.
ni hayo tu
ni hayo tu