Waandishi wafungiwa nje Bunge la Katiba

Waandishi wafungiwa nje Bunge la Katiba

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,883
Reaction score
1,482
index.jpg

Na Salome Kitomary 7th March 2014 Dk. Harrison Mwakyembe.

Bunge la Katiba limeamua kuweka kitanzi kwa uhuru wa wananchi kupata habari za mchakato wa Katiba Mpya, kwa kuwazuia waandishi wa habari kuingia kwenye Kamati 12 za wajumbe wa Bunge hilo zitakazojadili Rasimu ya Katiba.

Mjadala mkali ulizuka kwa juzi na jana kwenye Bunge hilo, huku baadhi ya wajumbe wakitaka uhuru wa wananchi kupata habari uwapo kwa waandishi kuruhusiwa kuingia kwenye kamati na wengine wakiwamo wajumbe wa Kamati ya Kanuni na Kumshauri Mwenyekiti wakipinga vikali kwa kutaka waandishi wapewe taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa kamati husika.

Kifungu cha 57 fasili ya kwanza ya Kanuni za Bunge Maalum la Katiba, kinaeleza kuwa vikao vyote vya kamati vitakuwa vya faragha na hakuna mtu yeyote asiyekuwa mjumbe wa kamati, mtumishi wa Bunge au mtaalam aliyeitwa na Mwenyekiti wa Bunge Maalum atakayeruhusiwa kukaa katika sehemu yoyote ya ukumbi wa mikutano ya kamati wakati kikao cha faragha kinaendelea.

Fasili ya tatu, inaeleza kuwa bila kuathiri masharti ya kanuni hii Mwenyekiti wa Kamati ya mjumbe yeyote kwa idhini ya Mwenyekiti anaweza kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu mambo yaliyojitokeza kwenye kikao cha kamati.
Baadhi ya wajumbe waliiomba kuwasilisha mapendekezo yao kwenye kifungu hicho, walitaka waandishi wa habari kuruhusiwa kwani kwa kuwazuia ni kwenda kinyume cha ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inayotaka kuwapo kwa uhuru wa kupata taarifa.

OLUOCH

Ezekiel Oluoch alisema anashauri vikao viwe wazi kwani hakuna jambo la siri la kujifungia kwani wananchi wana haki ya kujua kinachojadiliwa kwenye kamati na kwamba ni vyema kamati zikawa huru.

HALIMA MDEE

Halima Mdee alisema wenye jukumu la kuzitengeneza kanuni ni wajumbe na kwamba awali kamati ya kanuni na kumshauri mwenyekiti baada ya majadala mkubwa kamati ilipendekeza waandishi waruhusiwe kuingia kwenye vikao, na ikakubaliwa kwenye vikao vya kamati ambavyo vitakuwa na mijadala mikubwa na watakapokuja kwenye Bunge watafanya majumuisho kwenye manbo yaliyojadiliwa.

"Tulikubalina watu watakaokatazwa ni wananchi wa kawaida kutokana na
udogo wa kumbi, ila waandishi wa habari wakubaliwe, sisi ndiyo tunaopitisha kanuni na sisi tuliridhia ilikuwa ni matarajio yetu,"
alisema.

Alisema waliotajwa kwenye kanuni waruhusiwe kuingia na utaratibu utakaotumika uamuliwe na mwenyektii wa kamati kushauriana na makamu mwenyekiti.

"Waandishi wa habari waingie mnaogopa nini, mnaficha nini?…hii Katiba ni ya wananchi wana haki ya kujua kila kinachoendelea ndani ya kamati na nje ya kamati na kwenye ukumbi wa Bunge," alisema Mdee.

MOSES MACHALI

Moses Machali alipendekeza fasili ya tatu ya kifungu hicho, ifutwe kwa kuwa inaweka kitanzi kwa uhuru wa wananchi kupata habari na hakimlazimishi mwenyekiti au makamu kutoa taarifa kwa waandishi wa habari.

Alisema vikao vyote vifanyike kwa uwazi bila kuzuia mtu ingawa hawataruhusiwa kushiriki kwenye mjadala wa kamati.

"Hao wanaosisitiza kura ya wazi halafu mnaogopa na kuwakataa waandishi wa habari mnaficha nini, sioni sababu ya msingi," alisema Machali.

MARIA SARUNGI

Maria Sarungi alisema vikao vya kamati viwe wazi kwa waandishi wa habari kwa kuwa Rasimu ya Katiba itakwenda kwao kwa ajili ya kuipigia kura.

"Mwanzo wa Rasimu ya Katiba unasema kwakuwa sisi wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua…Katiba hii si ya kwetu tuliokaa humu ndani bali ya wananchi wa Tanzania, mchakato ulivyoanza ilianza kwa wananchi hadi tulipofika," alisema.

FREEMAN MBOWE

Freeman Mbowe alisema Katiba inayotungwa ni ya wananchi na wanaowakilishwa ndani ya Bunge hilo wanataka kujua kila kinachoendelea ndani ya Bunge hilo.

"Tusifikiri tunahitaji kuridhiana sisi wenyewe tulioko ndani ya Bunge hili kuna Watanzania kwa mamilioni wa vyama na taasisi mbalimbali wanatisikiliza," alisema.

Wakati wajumbe huyo anazungumza, baadhi ya wajumbe walipiga kelele na kuzomea hali iliyomlazimu kuacha kuzungumza na mwenyekiti kumsihi kuendelea, lakini Mbowe alisema: "Siwezi kuendelea wakati wajumbe wanapiga kelele."

MAHALU

Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na Kumshauri Mwenyekti wa Muda,Prof. Costa Mahalu, alisema kamati yake inapeleka mapendekezo kwa wajumbe na wenye maamuzi ni wajumbe na baadaye wanaagizwa kurekebisha mwafaka uliofikiwa na kuonyesha msimamo wao kwa pamoja.

Mjumbe wa Kamati, Bakari Khamis Bakari, alisema hakuna uhuru usiokuwa na kinga kulingana na maelezo ya maeneo husika na kwamba kamati italichukua suala hilo na kujadailiana ili kupata namna bora ya kuruhusu waandishi wa habari kuchukua habari.

George Simbachawene, mjumbe wa Kamati ya Kanuni na Kumshauri Mwenyekiti, alisema maoni ya kamati ni kuwa hisia na sababu wanazotoa wajumbe hao zilikuwapo kwenye kamati yao na walipenda waandishi waruhusiwe ili mchakato huo uonekane kwa umma wote.

"Kilichotushinda na kufikia uamuzi wa maoni hayo ni utekelezaji wake…kwa busara yetu tukaliwekea utaratibu kwenye fasili ya tatu, vyombo vyetu vya habari ni vingi, kamati iko ukumbi wa Msekwa asubuhi anakuja mwandishi anachukua anapeleka, habari zitakazokwenda juu ya hoja moja jambo moja zitakuwa hazijakamilika zitawachanganya wananchi na si kuwasaidia," alisema.

Alisema waandishi watachukua habari kivyao na kuwachanganya wananchi na ndiyo maana wameamua mwenyekiti wa kamati atoe taarifa kwa waandishi.

DK. MWAKYEMBE

Dk. Harrison Mwakyembe alisema kitaaluma ni mwandishi wa habari na mwanasheria na kwamba anaona hakuna haja ya waandishi wa habari kuruhusiwa kuwepo kwenye kamati na badala yake wapewa taarifa na mwenyektii wa kamati husika.

Hata hivyo, baadhi ya watoa hoja, walipinga hatua hiyo huku wanaopinga waandishi kuingia kwenye ukumbi wakishangilia kwa kupiga meza kusisitiza waandishi kunyimwa kuingai kwenye kamati hizo, huku wachache wa vyama wa upinzani wakipinga uamuzi huo.

DK. TULIA ACKSON

Mjumbe wa Kamati ya Kanuni na Kumshauri mwenyekiti, Dk. Tulia Ackson, alisema hakuna uhuru usiokuwa na mipaka na kwamba kamati inapendekeza kifungu hicho kubaki jinsi kilivyo.

Hoja hiyo ilimalizika kwa wajumbe kupitisha kifungu jinsia kilivyo kuwa waandishi hawataruhusiwa kuingia kwenye kamati na badala yake watapewa taarifa na mwenyektii wa kamati.

CHANZO: NIPASHE
 
Mimi nashangazwa na ccm kuendesha Bunge hili kwa vile watakavyo, Ikiwa Wamekataa kura katika Bunge isiwe ya siri, jee vipi leo waendeshe bunge hili kisiri siri bila Wananchi walio watuma kupata habari kutoka kwa wandishi wa habari?

Habari zakuja kupewa wandishi wa habari zitakua hazina laza yoyote, tunataka tuone live na kupokea habari up to date , ili tujuwe Wajumbe wetu tuliowachagua wanatusimamia vipi, au ni kwenda kula posha neno na kwenda miayo.

Ccm wamezoeya kujiamulia mambo watakavyo katika Bunge la Muungano sasa na hili wanataka kulitawala kisiasa na kuingiza itikadi za kivyama kulinda interest za chama chao.

Jee wamesahau kuwa hili ni Bunge la katiba na itikadi za vyama hazihusiki huku?

Wananchi tunataka tuone mijadala ALEVE si hivyo basi bunge halina maana na katiba itakayo tengenezwa itakua ni yagurupu la wala posha tu walomo ndani ya ukumbi.
 
Kakke,

..CCM wanataka kuendesha bunge hili kama kikao cha kamati kuu.

..waandishi wa habari waweke shinikizo kwamba lazima waingie ktk vikao vya kamati.

..ikiwezekana hata waweke mgomo mpaka pale bunge litakapopitisha uamuzi wa kuwaruhusu kuingia kwenye vikao vya kamati.

cc Pasco, Manyerere Jackton
 
Last edited by a moderator:

Mkuu JK, to be honest, sioni mantiki yoyote kwa waandishi kuzuiwa wanachofanya ni kufanya censorship ya jumla, ila practically, waandishi wenyewe na editors wao wangejikuta wanalazimika kufanya self censorship kwa sababu I can't imagine hao waandishi ambao wangeripoti majadiliano kwenye kamati toka kamati 12 za bunge hilo, kisha wakaja kuripoti taarifa rasmi ya wenyeviti wa kamati!, its automatically ma editors watasubiri taarifa rasmi za kamati ndipo waripoti!.
Ni uoga tuu wa bure usio na msingi wowote ndio unaowasumbua!.

Pasco
 
..and guess what?

..mmoja wa wajumbe aliyependekeza waandishi wazuiewe na Dr.Harison Mwakyembe.

..yaani amejisahau kabisa kwamba kabla hajajiunga UDSM kitivo cha sheria Mwakyembe alikuwa mwandishi wa habari.

..kwa kweli ukijiunga tu CCM your true colors become exposed. kama ulikuwa na hulka ya ufisadi ila unajificha ukijiunga CCM utakuwa fisadi tu. kama ulikuwa mwongo-mwongo lakini unaona haya au unamwogopa MUNGU ukijiunga CCM utasema uongo mchana kweupe.

cc Jasusi, Mchambuzi, Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
Kina Mwakyembe wameshalamba asali ya kisiasa, hawakumbuki tena shubiri ya uandishi. Wameshashiba, hawajali wenye njaa.
 
Dr. HM alikuwa mwalimu wangu pale UD kiukweli jamaa ni just too sensationa!. Ilipodaiwa kalishwa sumu, niliwapinga watu humu, nikawaambia its good if comes clean!, he never na watu mpaka kesho hawajui!. Its was just his make-up!.

Kuna hoja kuwa hakuna absolute press freedom popote, alipotaja change of rule of engagements, nilidhani atasema suala la katiba ni la watu, na wao ni wawakilishi tuu, hivyo nilitegemea angesema watu wana haki kujua kila kinachoendelea!.

Hili bunge pia litatusaidia kuwajua men of integrity from mediocre!. Ndani ya CCM kuna men of integrity ambao hawakubaliani na madudu ya CCM, kuliko kujidhalilisha, wameamua bora wajinyamazie kutunza heshima zao!.

Pia bunge hili linatufungua macho kuyaona madebe matupu!.
Pasco.
 
Kina Mwakyembe wameshalamba asali ya kisiasa, hawakumbuki tena shubiri ya uandishi. Wameshashiba, hawajali wenye njaa.

..kwenye nchi za wenzetu wanasiasa hawadharau waandishi wa habari kama inavyofanyika hapa Tanzania.

..mwenzenu Mwangosi aliuawa kule Iringa, na kamanda wa Polisi aliyesimamia zoezi lile amepandishwa cheo, lakini waandishi wa habari mmekaa kimya.

cc Pasco
 
Last edited by a moderator:
..and guess what?

..mmoja wa wajumbe aliyependekeza waandishi wazuiewe na Dr.Harison Mwakyembe.

..yaani amejisahau kabisa kwamba kabla hajajiunga UDSM kitivo cha sheria Mwakyembe alikuwa mwandishi wa habari.

..kwa kweli ukijiunga tu CCM your true colors become exposed. kama ulikuwa na hulka ya ufisadi ila unajificha ukijiunga CCM utakuwa fisadi tu. kama ulikuwa mwongo-mwongo lakini unaona haya au unamwogopa MUNGU ukijiunga CCM utasema uongo mchana kweupe.
Unajua ndani ya bunge hilo kuna wazalendo ambao watatupa taarifa za kina.
Endapo mambo ya kamati kuu yenye watu 22 yanatoka hilo la bunge la katiba litakuwa wazi tu.

Jambo la hatari zaidi ambalo waheshimiwa hawalioni ni upotoshaji wa habari kutokana na habari hizo kupitia njia za panya.
Ni suala la muda tu utaona thread zikisema ' Mbunge A ataka kipengele cha ushoga' Mbunge huyo hatakuwa na platform ya kueleza anachokusudia kwasababu hakuna njia rasmi. Kama ni katika magazeti atakuwa na nafasi ya kuhoji na hata kuchukua hatua.

Ni kwamba wanachokifanya ni kuruhusu 'public' kuwa media na kila mtu atakuja na lake at their costs.

Lakini pia linatoa mwanga kuwa process yote umegubikwa na uhuni na uhalifu. Kwanini bunge linalolipwa kwa pesa za walipa kodi lifanya mambo nyuma ya pazia. Kuna nini?
 
..kwenye nchi za wenzetu wanasiasa hawadharau waandishi wa habari kama inavyofanyika hapa Tanzania.

..mwenzenu Mwangosi aliuawa kule Iringa, na kamanda wa Polisi aliyesimamia zoezi lile amepandishwa cheo, lakini waandishi wa habari mmekaa kimya.

cc Pasco
Waandishi walitakiwa wae kitu kimoja. Hawana hilo kwasababu ya bahasha za khaki. Leo wanatupwa nje kesho wapo makanisani na miskitini na wagombea watarajiwa wakiwapamba.

Kwa nchi za wenzetu habari kuu ingekuwa Kuhusu wahuni walioamua kujifungia ili kutekeleza azma ya uhuni.
 
Dr. HM alikuwa mwalimu wangu pale UD kiukweli jamaa ni just too sensationa!. Ilipodaiwa kalishwa sumu, niliwapinga watu humu, nikawaambia its good if comes clean!, he never na watu mpaka kesho hawajui!. Its was just his make-up!.

Kuna hoja kuwa hakuna absolute press freedom popote, alipotaja change of rule of engagements, nilidhani atasema suala la katiba ni la watu, na wao ni wawakilishi tuu, hivyo nilitegemea angesema watu wana haki kujua kila kinachoendelea!.

Hili bunge pia litatusaidia kuwajua men of integrity from mediocre!. Ndani ya CCM kuna men of integrity ambao hawakubaliani na madudu ya CCM, kuliko kujidhalilisha, wameamua bora wajinyamazie kutunza heshima zao!.

Pia bunge hili linatufungua macho kuyaona madebe matupu!.
Pasco.
Pasco tululipokuwa tunasisitiza kura ya wazi maana yake ilikuwa kutoa fursa ya kuwafahamu wahuni, wahalifu, wanafiki, vigeuge na wapuuzi wengine katika makundi hayo.

Leo hao wanaotaka kujifungia kuandika nyaraka ya umma kwa siri eti wanataka urais. Tutaambiwa wana sura njema na kauli tamu, ni wame sana katika kugawa khanga na blazia, pilau na kofia. Wanatufaa!
Mwisho wa siku tunaaangalia nyuma na kusikitika.

Bunge ni sehemu ya wazi isiyohitaji kificho cha aina yoyote. All in all tutapata habari tu za huko walikojifungia.
Tutajua nani kasema nini na tutamwagia mafuta ya petroli iwe ukweli au uongo. Habari itakayoletwa itakuwa sahihi kwasababu hatuna chanzo cha kitaaluma.

Ngoja baada ya siku tatu tutasikia wote wanaoomba vyeo, posho wanaotaka kuuza nchi na wanaotaka ubia wa kununua nchi. Tutawapindisha na kwajadili bila huruma.
 
..and guess what?

..mmoja wa wajumbe aliyependekeza waandishi wazuiewe na Dr.Harison Mwakyembe.

..yaani amejisahau kabisa kwamba kabla hajajiunga UDSM kitivo cha sheria Mwakyembe alikuwa mwandishi wa habari.

..kwa kweli ukijiunga tu CCM your true colors become exposed. kama ulikuwa na hulka ya ufisadi ila unajificha ukijiunga CCM utakuwa fisadi tu. kama ulikuwa mwongo-mwongo lakini unaona haya au unamwogopa MUNGU ukijiunga CCM utasema uongo mchana kweupe.

cc Jasusi, Mchambuzi, Nguruvi3

Mwakyembe aliapa kuilinda na kuitetea katiba ya "Jamhuri ya muungano wa Tanzania".

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Dr. HM alikuwa mwalimu wangu pale UD kiukweli jamaa ni just too sensationa!. Ilipodaiwa kalishwa sumu, niliwapinga watu humu, nikawaambia its good if comes clean!, he never na watu mpaka kesho hawajui!. Its was just his make-up!.

Kuna hoja kuwa hakuna absolute press freedom popote, alipotaja change of rule of engagements, nilidhani atasema suala la katiba ni la watu, na wao ni wawakilishi tuu, hivyo nilitegemea angesema watu wana haki kujua kila kinachoendelea!.

Hili bunge pia litatusaidia kuwajua men of integrity from mediocre!. Ndani ya CCM kuna men of integrity ambao hawakubaliani na madudu ya CCM, kuliko kujidhalilisha, wameamua bora wajinyamazie kutunza heshima zao!.

Pia bunge hili linatufungua macho kuyaona madebe matupu!.
Pasco.

Tayari limeisha tufungua macho na madebe matupu mengi tumeyaona na jambo la kusikitisha yapo ktk ngazi ya juu ktk Serikali ya JMT akiwemo huyu mwalimu wako bingwa wa maigizo na mazingaombwe!
 
Back
Top Bottom