Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera amewashauri waangalizi wa ndani wa uchaguzi kuwa na fedha ili wawe na uwezo wa kufanya kazi hiyo badala ya kutegemea wafadhili.
Ametoa kauli hiyo leo wakati NEC ilipokutana na kufanya mazungumzo na watazamaji wa uchaguzi ndani na nje na kuwaelezea jinsi Tume ilivyojiandaa kwa uchaguzi, wakati wao wakilia na changamoto ya upatikanaji wa fedha.
Akizungumza na wanahabari, Dk Mahera amesema baadhi ya watazamaji wa ndani walisema hawajapata fedha kutoka kwa wafadhili kwa ajili ya kushiriki uchaguzi.
“Hata sisi wenyewe uchaguzi huu tumetegemea Serikali, hatukuomba fedha nje. Bajeti yetu ilikuwa Sh331 bilioni kwa ajili ya uchaguzi na zote Serikali imetoa na wao sasa hawakupata fedha kutoka kwa wafadhili,” alisema.
“Hivyo watazamaji wa ndani ni vizuri wakati mwingine kujiandaa vizuri kuweza kutafuta fedha kwa ajili ya kutazama na kwa bajeti ambazo ni za kawaida kwa mazingira yetu ya Tanzania ili waweze kutazama uchaguzi na hatimaye kutoa taarifa.
“Kwa hawa watazamaji wa nje wao walikuwa na fedha hawana matatizo yoyote.”
Katika mkutano huo pia tume iliwaeleza watazamaji namna maandalizi ya uchaguzi yalivyofanyika kuanzia kuandikisha wapigakura, ununuzi wa vifaa vya uchaguzi, uteuzi wa watendaji, wagombea na usimamiaji wa kampeni zinazoendelea na usambazaji wa vifaa katika ngazi ya majimbo.
Maulid Mkwati, mmoja wa waangalizi wa uchaguzi, aliitaka Tume kuandaa semina hata ya siku moja ili kuwafundisha namna nzuri ya kufanya kazi kwa ufanisi, ikiwemo uandaaji mzuri wa madodoso.
“Haya madodoso tunaweza kuyaandaa sisi kumbe kuna kitu tumekisahau, hivyo nilifikiri Tume ingeandaa hata siku moja kutupatia semina kutufundisha haya au ungeandaliwa mfumo ambao tungeweza kutumia kukusanya maoni yetu ingependeza zaidi kuliko kila mtu kutegemea mfumo wake,” alisema.
“Pia changamoto ya bajeti ilikuwa ni kubwa. Nafikiri hapa wote tunalia fedha. Tulitegemea kuwa tukikosa fedha za wadau tungewezeshwa.”