Waangalizi wa uchaguzi Kenya waanza kuzungumza na timu ya Raila Odinga

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Waangalizi wa kimataifa wa Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Madola wametoa ripoti yao ya awali kuhusu uchaguzi Kenya na mazungumzo yao na kambi ya upinzani ya National Super Alliance (Nasa) waliowasilisha madai kwamba kompyuta za IEBC zimeingiliwa na upande Jubilee kuvuruga matokeo halisi ya kura.


Kiongozi wa ujumbe wa Waangalizi wa Umoja wa Afrika, Thabo Mbeki alisema ni kweli mgombea wa Nasa, Raila Odinga na ujumbe walikutana nao wakiwa na nyaraka za madai kuhusiana na Jubilee walivyovamia kompyuta hizo.
Mbeki alisema waliwasikiliza na kuwaeleza kuwa watalifikisha suala hilo IEBC. Hata hivyo alisema Nasa walitaka waangalizi hao wafanyanyie kazi nyaraka hizo kwa kuchunguza.


"Kwa mtu kama sina utaalamu wa teknolojia kuniambia nichunguze ni sawa na kuniambia nifanye kazi ambayo sina ujuzi," alisema Mbeki.
Alisema kazi ya waangalizi ni kuangalia ni si kuchunguza, kwa kuwa wao jukumu lao ni kuangalia namna mchakato mzima ulivyofanyika kama ulifuata sheria za nchi husika na taratibu za kuheshimu demokrasia walizojiwekea katika Umoja wa Afrika.


Alisema tuhuma zote zilizotolewa na Nasa wameziwasilisha kwa mamlaka husika ndani ya Kenya.
Kwa upande wake mkuu wa ujumbe wa waangalizi wa Jumuiya ya Madola, Rais wa zamani wa Ghana, John Dramani Mahama alisema walikutana na Odinga na ujumbe wake na walitoa madai ya kompyuta za IEBC kuvamia huku wakiwa na nyaraka kama ushahidi wa madai yao, hata hivyo Mahama alisema nao waliwaeleza kwanza hawana utaalamu wa teknolojia hiyo, lakini jukumu lao ni kuangalia kama utaratibu mzima wa uchaguzi umefuata sheria na katiba ya nchi na madai mengine ya ukiukwaji wa taratibu yana utaratibu wake uliowekwa kwa mujibu wa sheria

.
 
Kitendo cha watu wanaoheshimika sana duniani kuwa waangalizi wa uchaguzi wa Kenya maana yake nini ?
 
Kama anadai itakuwa mara ya 4 ,na kulingana na Uhuru Kenyatta,kosa ni la Raila Odinga.
 
Kwa nini Marais wastaafu wa Tanzania huwa hawapewi hizi kazi za usimamizi za Jumuiya ya Madola................!!?

Sikumbuki kumsikia Kikwete, Mkapa wala Mzee Mwinyi!!
 
Kwa nini Marais wastaafu wa Tanzania huwa hawapewi hizi kazi za usimamizi za Jumuiya ya Madola................!!?

Sikumbuki kumsikia Kikwete, Mkapa wala Mzee Mwinyi!!
Bora Kikwete ana utu kidogo ila Mkapa ni sawa na DAB, Mwinyi nae hajielewi mimi sijui hata urais aliupataje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee Raila akubali jua limeshazama basi.... Mengineyo umri umesogea apumzike. Baba yake nae alijaribu ulifika wakati akakubali jioni huwa inafika akapumzika. Kama ipo ipo yule mstaafu wa Gambia pamoja na udikteta wake lkn box la kura liliongea akatoka zake.... Sasa kwa Mr Raila, Mungu awasaidie tu wakenya.

"A voice of one calling in the wildernes"
 
Kwa nini Marais wastaafu wa Tanzania huwa hawapewi hizi kazi za usimamizi za Jumuiya ya Madola................!!?

Sikumbuki kumsikia Kikwete, Mkapa wala Mzee Mwinyi!!
Kikwete alikuwa Kiongozi wa waangalizi wa Kimataifa kwenye Uchaguzi wa hivi karibuni wa Zambia..
Ila sikumbuki alikuwa anawakilisha Jumuiya ya Madola, SADC au Jumuiya ipi.
 
Pole sana Raila Odinga kweli matokeo yamechakachuliwa tafadhali fanya mpango wa marekebisho ya katiba ili uchaguzi ujao ifanyike kura ya mlolongo kama enzi za Rais Moi huyu mtindo wa sasa unapigwa na hujui unapigiwa wapi.
Pole sana baba
 
Kwa nini Marais wastaafu wa Tanzania huwa hawapewi hizi kazi za usimamizi za Jumuiya ya Madola................!!?

Sikumbuki kumsikia Kikwete, Mkapa wala Mzee Mwinyi!!
Mkapa kwa sasa ni msuruhishi wa mzozo wa burundi, hivyo hawezi kupewa jukumu jingine la kimataifa kubwa kama hilo!

Na kwa sababu tz tayari ina usuruhishi kwenye nchi nyingine, sio vibaya wawakilishi wa mataifa mengine wakapewa nafasi!

Lakini pia Mkapa alikuwa ni mmoja wa wasuruhishi wa machafuko kenya ya 2007/2008, yeye na Koffi Anan.
 
Hizi nafasi za uangalizi wangepewa akina joti, mpoki, irene Uwoya na harmorapa ingependeza sana na ingetuletea taifa sifa kubwa sana kuliko njemba zee akina mkapa inayongangania kuishi badala wapumzike kuzimu where they truly belong.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…