Waarabu, Wazungu walivyochangia kukua na kuenea Kiswahili

Waarabu, Wazungu walivyochangia kukua na kuenea Kiswahili

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
KWA UFUPI

Dini: Dini ilichangia ueneaji wa lugha ya Kiswahili kupitia mawaidha na mafunzo ya madrasa. Waarabu walipokuja walitaka kueneza dini ya Kiislamu katika maeneo waliyofikia.



Katika karne ya 19, Afrika Mashariki iliingia kwenye uhusiano na mataifa mengine kama vile Ujerumani na Uingereza.

Uhusiano huo ni baada ya watu wa pwani kuwa na uhusiano wa muda mrefu wa kibiashara na Waarabu. Hawa waliweka athari kubwa katika kukua na kuenea kwa lugha ya Kiswahili.

Wageni kutoka Ulaya walipoingia Afrika Mashariki walifanya biashara, shughuli za kidini elimu na utawala.

Kama ilivyokuwa katika kipindi cha Waarabu, uwapo wao pia ulikuwa na athari katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili Afrika Mashariki na kwingineko.

Kipindi cha Waarabu

Waarabu hasa katika pwani ya Afrika Mashariki walifanya biashara, ikiwamo biashara ya watumwa. Ilikuwapo misafara mbalimbali ya biashara kutoka pwani hadi bara. Katika misafara hiyo Kiswahili ndiyo iliyokuwa lugha ya mawasiliano hivyo Kiswahili kikaenea pia katika sehemu za bara.

Kuna mambo kadhaa waliyofanya Waarabu ambayo yalichangia kukua kwa lugha ya Kiswahili. Waarabu walichangia kukua kwa lugha ya Kiswahili kama ifuatavyo:

Biashara: Waarabu walifanya biashara kati ya pwani na sehemu za bara, katika biashara yao walichangia uenezaji wa lugha ya Kiswahili. Lugha kuu ya mawasiliano na ya kibiashara iliyotumiwa na wafanyabiashara wa Kiarabu ilikuwa ni Kiswahili.

Kwa hiyo kwa njia hii waliweza kueneza Kiswahili kuanzia pwani hadi maeneo ya bara kama vile Morogoro, Dodoma, Tabora, Kigoma hadi Mashariki mwa Kongo.

Dini: Dini ilichangia ueneaji wa lugha ya Kiswahili kupitia mawaidha na mafunzo ya madrasa. Waarabu walipokuja walitaka kueneza dini ya Kiislamu katika maeneo waliyofikia. Hivyo, walianzisha madrasa ambayo walitumia kufundisha huku wakitumia lugha iliyokuwa ikitumiwa ambayo ni lugha ya Kiswahili.

Maandishi ya Kiarabu: Waarabu pia walileta hati zao zilizotumiwa katika maandishi ya lugha ya Kiswahili. Kwa hiyo kupitia hati za Kiarabu maandishi mbalimbali ya lugha ya Kiswahili yaliweza kuhifadhiwa. Hivyo Kiswahili kilikua kutokana na kuhifadhiwa katika maandishi na kusomwa wakati wowote.

Kuoana: Vilevile Waarabu waliofika pwani waliweza kuoana na Wabantu. Hii ilisababisha kuzaliwa kwa watoto ambao walizungumza lugha ya kati kutoka kwa wazazi wao. Na kwa sababu hiyo watoto walichukua maneno mengi kutoka kwa baba na mama yao na hivyo kusababisha kuzungumza lugha Kiswahili. Kipindi cha Wajerumani
Wajerumani waliingia pwani ya Afrika Mashariki mwaka 1875, walifanya kila jitihada kuwatawala Waafrika na katika utawala wao pia walifanya biashara, waliendesha shughuli za kiutawala, kidini na kielimu. Katika shuguli zote hizo Kiswahili ndiyo ilikuwa lugha ya mawasilino hivyo kukikuza na kukiendeleza Kiswahili.

Wakoloni wa Kijerumani waliwalazimisha wafanyakazi wa Serikali kujifunza Kiswahili ili wapate ajira katika utawala huo. Kwa hiyo suala hili lilisababisha watu kujifunza lugha ya Kiswahili ili waweze kuajiriwa. Wafanyakazi nao ilikuwa ni lazima wajifunze Kiswahili.

Wajerumani pia walilazimika kujifunza Kiswahili ili waweze kuwasiliana na wenyeji kwa urahisi ili kurahisisha shughuli zao za kiutawala. Shule zilifunguliwa za kufundisha watu weusi ili wawe wasaidizi wao katika utawala wa Wajerumani. Itaendelea

Mwandishi ni mtaalamu wa Kiswahili na mhakiki wa lugha wa gazeti hili. chanzo.Waarabu, Wazungu walivyochangia kukua na kuenea Kiswahili - Makala - mwananchi.co.tz


HONGERA WAARABU NA WAZUNGU KWA KUISAMBAZA LUGHA YA KISWAHILI.

 
Back
Top Bottom