Sikiliza. Mikopo ni kama vidonge. Kila mkopo na matumizi yake na kila tatizo na aina yake ya mikopo.
Tafuta kwanza benki inayotoa mikopo ya kilimo upate kujua huduma zao na mahitaji ua huduma zile.
Kama vile usivyoweza kulazimisha sumu ya panya, ambayo ni muhimu sana katika kukabiliana na panya itumike kuhifadhia karanga, au kama vile suivyoweza kulazimisha dawa ya mseto ambayo ni kwa Malaria itumike kama Nusu kaputi kweny eoperation, vile vile huwezi kulazimisha mkopo uliobuniwa kwa ajili ya biashara za kununua na kuuza bidhaa, utumike katika kilimo. Hapo hutaweza kunufaika nao, wala kurejesha na hivo kuanza kutukana mabenki. Hata hao Bankers pia sidhani wanapenda kugombana na mteja wao, na pia hawapendi biashara yao ianguke, ndiyo sababu ukikutana na banker makini atakushauri aina ya huduma inayofaa kwa hitaji lako.
Kwa ufupi tafuta bank zinazokopesha kwa ajili ya kililmo kwa sababu mikopo yao itakuwa imezingatia hali ya kilimo kwa Tanzania kwa maana ya mhula wa mkopo, muda wa urejeshaji, muda wa uchukuaji, kipindi cha neema, na hata uwezekano wa refinancing kwa kutokana na kilimo labda kutegemea hali ya hewa, na uhaba wa irrigation infrastructure, na mabadiliko ya tabia ya nchi, unachotaka kukilima, tekinolojia unayotumia, gharama zako katika uzalishaji, soko la bidhaa zako, bei tarajiwa za mazao yako, msimu wa mauzo n .k.
Kuhusu tathmini ya dhamana yako, ni vizuri uwe na tathmimi yako ambayo pia bankers wataithibitisha kwa kuwa mwisho wa siku wewe na bankers mtakuwa wadau wa hiyo dhamana kwa kpindi chote cha mkopo.
Usiogope kuwa mkwei na muwazi ili upate huduma sahihi. Afadhali kuwa mkweli katika udhaifu ili ukose mkopo usio sahihi kuliko kupata mkopo kwa udanganyifu ambao mwisho wake utakupa hasara na majuto.
Kama una swali zaidi uliza.