Waatalamu wa mikopo naomba msaada

A2G

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2016
Posts
283
Reaction score
829
Habari za majukumu wakuu

Kwa mwenye ufahamu au mtaalamu wa mikopo naomba kujua Kama inawezekana kutumia kiwanja kilicho pimwa kama dhamana ya kupata mkopo Benki kwa ajili ya mradi wa kilimo.

Kama inawezekana ningependa kujua pia Kama benki wenyewe ndio watafanya valuation ya kiwanja kujua thamani yake au hiyo natakiwa kufanya mwenyewe
 
Benki nyingi ukiwaambia unaenda kufukia hela wanakuwa na mtazamo hasi kwamba hutolipa.
Hilo moja, LA pili kiwanja kilicho tupu bila hata msingi ni vigumu kukubalika kama dhamana, walau upandishe hata vitofali sita.

Lakini huenda kuna taasisi utafanikiwa ngoja waje wadau

Kwa Hisani Ya Watu Wa Mbeya!
 
Swali lako hapa ni nani anafanya valuation kati yako na benki?

Kimsingi anayetoa hela ndiyo a nathaminisha dhamana.maana yake ni bei ya soko toa asilimia 20 au 40 au wakati mwingine 50. So ninavyojua hao watu wa benki wanawathamini wao
 
Reactions: A2G
Swali lako hapa ni nani anafanya valuation kati yako na benki?

Kimsingi anayetoa hela ndiyo a nathaminisha dhamana.maana yake ni bei ya soko toa asilimia 20 au 40 au wakati mwingine 50. So ninavyojua hao watu wa benki wanawathamini wao

Una maanisha hivi

Thamani = bei ya soko ya dhamana - (20%/40%/50% * bei ya soko ya dhamana)

Au nimeelewa vibaya?
 
1. Kiwanja unaweza kutumia kama dhamana lakini inategemea na eneo la kiwanja na namna gani eneo hilo lilivyo 'potential'
2. Suala la kuthaminisha thamani ya kiwanja hufanywa na benki wenyewe kwa kuwatumia wathaminishaji ardhi waliosajiliwa kisheria. Hivyo nao huangalia bei ya soko ilivyo kwa kiwanja chako, eneo kilipo, ukubwa na umuhimu wa eneo lenyewe kwa mfano iwapo ukashindwa kulipa mkopo je kinaweza kuuzika kwa urahisi na uharaka kwa kiasi gani kwa mahusiano na matumizi ya eneo hilo
3. Kuna baadhi ya mabenki wana mlango huo wa mikopo ya kilimo. Lakini kilimo chako ni cha mazao ya chakula au mazao ya biashara? Mazao ya biashara unaweza kupata mkopo, pili katika shamba lako shughuli za kilimo zinaendelea au ndo wataka kuanza na tatu ukubwa wa shamba lako nao ni kigezo. Maana usiende kutafuta mkopo wakati shamba lako halipo katika levo ya 'plantation' bali ni 'farm' tu
4. Baadhi ya benki zitoazo mkopo kupitia kilimo pita upate maelezo zaidi ni NMB, TIDB na mabenki mengine hukubali kukupa mkopo kupitia biashara nyingine lakini lengo la mkopo ikiwa ni katika shughuli za kilimo
Nawasilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Sikiliza. Mikopo ni kama vidonge. Kila mkopo na matumizi yake na kila tatizo na aina yake ya mikopo.

Tafuta kwanza benki inayotoa mikopo ya kilimo upate kujua huduma zao na mahitaji ua huduma zile.

Kama vile usivyoweza kulazimisha sumu ya panya, ambayo ni muhimu sana katika kukabiliana na panya itumike kuhifadhia karanga, au kama vile suivyoweza kulazimisha dawa ya mseto ambayo ni kwa Malaria itumike kama Nusu kaputi kweny eoperation, vile vile huwezi kulazimisha mkopo uliobuniwa kwa ajili ya biashara za kununua na kuuza bidhaa, utumike katika kilimo. Hapo hutaweza kunufaika nao, wala kurejesha na hivo kuanza kutukana mabenki. Hata hao Bankers pia sidhani wanapenda kugombana na mteja wao, na pia hawapendi biashara yao ianguke, ndiyo sababu ukikutana na banker makini atakushauri aina ya huduma inayofaa kwa hitaji lako.

Kwa ufupi tafuta bank zinazokopesha kwa ajili ya kililmo kwa sababu mikopo yao itakuwa imezingatia hali ya kilimo kwa Tanzania kwa maana ya mhula wa mkopo, muda wa urejeshaji, muda wa uchukuaji, kipindi cha neema, na hata uwezekano wa refinancing kwa kutokana na kilimo labda kutegemea hali ya hewa, na uhaba wa irrigation infrastructure, na mabadiliko ya tabia ya nchi, unachotaka kukilima, tekinolojia unayotumia, gharama zako katika uzalishaji, soko la bidhaa zako, bei tarajiwa za mazao yako, msimu wa mauzo n .k.

Kuhusu tathmini ya dhamana yako, ni vizuri uwe na tathmimi yako ambayo pia bankers wataithibitisha kwa kuwa mwisho wa siku wewe na bankers mtakuwa wadau wa hiyo dhamana kwa kpindi chote cha mkopo.

Usiogope kuwa mkwei na muwazi ili upate huduma sahihi. Afadhali kuwa mkweli katika udhaifu ili ukose mkopo usio sahihi kuliko kupata mkopo kwa udanganyifu ambao mwisho wake utakupa hasara na majuto.

Kama una swali zaidi uliza.
 
Reactions: A2G

Nashukuru sana mkuu. Kimsingi Mimi nimeshalima msimu uliopita nikaona Changamoto kubwa ipo kwenye matumizi ya manual work hivyo inapunguza production kwahiyo nataka nipate mkopo ninunue mashine ya kazi.

Nina viwanja viwili kimoja kipo barabarani lakini hakujapimwa nataka nipime nipate hati ya makazi na biashara. Kingine kina hati Ila kipo 1.5km kutoka barabarani na maji na umeme havijafika kwahiyo nitaangalia kipi kina thamani zaidi kwa benki kwa maana ya market value na kuuzika kirahisi

Lakini pia nafikiria kufanya contract farming ili benk ipate uhakika kuwa Nina mnunuzi tayari wa mazao yangu ili kuongeza sifa za kuupata mkopo.
 

Ubarikiwe kiongozi kwa point yako ya msingi kuhusu uchaguzi wa aina ya mkopo. Nimerudi mjini Jana nikafanikiwa kwenda TIB wakanishauri niende benki ya kilimo huko ndio naweza kupata mikopo sahihi zaidi Kama usemavyo

Acha nipambane nitaleta mrejesho ili uwanufaishe na wengine
 
Vizuri Mkuu
Vile vile jaribu kuna taasisi inaitwa EFTA TANZANIA wanatoa mikopo ya mashine tu sio pesa. Vigezo vyao havipo tight sana. Wateja wetu baadhi wamepata mikopo huko ya vifaa vya kazi katika shughuli za kilimo. Muhimu uwe na maandiko yanayotakiwa
Nawasilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Reactions: A2G
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…