Waathirika wa Coronavirus wafikia 281

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe ametangaza visa vipya 11 vya COVID-19 nchini humo na idadi ya waathirika wa ugonjwa huo imefikia 281.

Wagonjwa wapya wote hawajasafiri siku za hivi karibuni, na watatu waliotokea Mombasa walikuwa karibu na Mgonjwa wa Corona aliyepoteza maisha wiki moja iliyopita

Mbali ya ongezeko la waathirika nchini humo, imetangazwa kuwa wagonjwa wawili wa COVID-19 wamepona na jumla ya waliopona nchini humo hadi sasa ni 69

Watu wapatao 13,872 wamepimwa tangu Virusi vya Corona viripotiwe kwa mara ya kwanza nchini humo

Idadi ya waliofariki dunia imebakia 14 na hakuna vifo vipya vilivyoripotiwa

======


Kenya has tested an additional 11 cases of the new coronavirus, bringing the tally to 281.

The cases are aged between 11 and 80 years old.

Seven of the new cases are from Mombasa; 3 from Bondeni, 1 from Miritini and three others from other parts of Mombasa town.

The rest of the four cases are from Nairobi.

Five of the new cases are from persons currently in government isolation centres while the rest were picked by the government’s surveillance team.

Ministry of Health CS Mutahi Kagwe noted that the infected persons do not have any recent travel history.

Three of the infections from Mombasa are the contacts of the herbalist who succumbed to the virus a week ago.

At the same time, two patients among them a doctor have recovered from the virus.

The total number of those who have recovered so far is 69 while the number of fatalities from the virus remains 14 people.

Kenya has so far tested 13872 samples since the first case was reported.


Source: Citizen TV
 
Mpaka sasa waliopimwa ni Kenya ni 13,872
Wakenya tuendelee kukumbushiana, hiki kitu kiko mtaani kimezagaa na kutamalaki, tuchukue tahadhari, kunao bado hatuonekani kujali, vijana bado wanakusanyika na kusongamana kwa makundi, jameni hiki kirusi ni ile tu kinaonekana kuwa na huruma kwa Waafrika maana sioni kikubwa tunachokifanya ambacho tunaweza tukasema ndio sababu kuu hatufi kwa mamilioni Afrika.

Ndio maana baadhi ya mataifa ya Kiafrika yameamua kukaidi ushauri wowote na kutokuchukua tahadhari yoyote, wapo wapo tu.
 
Hio ni sawa na 0.04% ya population ya Kenya.

Vipi tutamaliza lini? au siku tunamaliza wale waliopimwa mwanzo hali zao zitakuwaje🙂


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hio ni sawa na 0.04% ya population ya Kenya.

Vipi tutamaliza lini? au siku tunamaliza wale waliopimwa mwanzo hali zao zitakuwaje🙂



Sent using Jamii Forums mobile app

Hatupimi tumalize, hakuna nchi yenye uwezo wa kumaliza kupima hata wale wenye uchumi mara 1,000 zaidi yenu.
Tunapima kwa kutumia mikakati.
Nyie naona ile 53 ya juzi ilisababisha mtafaruku kwa wakuu hadi wameamua kuufyata, hawataji tena, waziri wenu sijui nini kilimuingia ghafla akaamua kusema ukweli, mpaka mwenyewe akajisema sehemu kwamba ameamua kusema ukweli.......
Zanzibar wameachiwa uwanja waendelee kutaja taja idadi yao.

Hiki kitu kinapaswa kutajwa kama kilivyo, hata mabingwa wa usiri akina Iran, Urusi hata mapanki wa Korea Kaskazini wameamua kutaja tu.
 
Yetu imetoka tena leo, sasa tuko 254. Mapambano bado yanaendelea...
Nasikia huko sasa mme-abandon "mass testing🙂


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mumetuzidi kwa active cases maana kwetu 69 wamepona.
Hayo " umeskia" hatuwezi kuyajadili.
Ugonjwa huu sio wa kukamiana, naona kuna ka ligi flani ya baadhi ya Wakenya na Watanzania....hivi tuna ubavu wa kuchekana?
Tuache huo ujinga. Wakenya wasipokuwa salama Watanzania hatuko salama pia
Hio ni sawa na 0.04% ya population ya Kenya.

Vipi tutamaliza lini? au siku tunamaliza wale waliopimwa mwanzo hali zao zitakuwaje🙂



Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutangulia sio kufika hivyo msijififu, tupeni muda watanzania tutawafikishia idadi hiyo na kuzidi baada ya siku chache tu

Huku raisi wetu yuko kwao, nchi yetu kamkabidhi bwana yesu na wachungaji wahangaike nayo

Huu ni mzaha, na hatuko tayari kuona usaha
 
Yaani unamsubiri rais akuchape kwanza kabla ya kuchukua tahadhari?
 
Jamani tuchekane kwenye mengine siyo huu ugonjwa. Tena kwenye hili tungejulishaba cultural practice ikiwemo tiba asilia maana tukifuata njia za magharibi tutakufa.
 
Yaani unamsubiri rais akuchape kwanza kabla ya kuchukua tahadhari?
Kipindi hiki hakuna tahadhari ambayo ikichukuliwa inaweza kuleta impact yeyote

Tahadhari iliyotakiwa kuchukuliwa mapema ambayo ingezaa matunda, ilikua ni kuzuia wageni wasiingie pamoja na kufunga mipaka kipindi ambacho hakukua na muathirika
 
Hilo dongo la mwisho ni la kwetu au...?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…