Marjo Mlekwa
Member
- Jul 18, 2021
- 38
- 60
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri na mapambano dhidi ya dawa za kulevya yaendelee!!
Kutana na kijana Mtanzania Faraja, umri wake ni miaka 23, hakumaliza masomo yake kwenye chuo cha sanaa Bagamoyo, sababu kubwa ikiwa ni msukumo na ushawishi mbaya wa vijana wenzake ambao siku zote aliamini kuwa ndio marafaiki zake wa kweli.
“muda mwingi nilikuwa nautumia kwa washikaji zangu Kinondoni” Hili ni jibu alilonipa Faraja wakati nilipomuuliza swali la Ilikuaje akajiingiza kwenye Matumizi ya dawa za kulevya ambayo kimsingi tayari yalikuwa yameshaharibu afya yake na hata ndoto yake kubwa ya kuwa muigizaji na muongozaji wa filamu.
Rangi ya mwili wake ya maji ya kunde ilikuwa na taswira nyingine tofauti kwa sababu ya kutofanyiwa usafi mara kwa mara, alikuwa na rasta fupi ambazo zilikuwa na muonekano mbaya usioridhisha macho ya yeyote anayemtazama, midomo yake ilikuwa na utando mweupe na usingependelea kuitazama kwa muda mrefu, Sauti yake ilikuwa ikikoroma kwa kuchoshwa na mihadarati, Shati lake la mikono mifupi lililochoka kwa uchafu lilisababisha majeraha ya sindano yaonekane kwa wingi kwenye mikono yake.
Kijana mwenzangu kuwa katika hali hii ni pigo la huzuni kwenye mtima wangu, ikanirudia pia kumbukizi ya Ripoti ya hivi karibuni iliyotolewa na umoja wa mataifa kitengo kinachohusika na dawa na uhalifu UNODC ambayo imeonesha idadi ya wanaoutimia Mihadarati Duniani inaongezeka na kwa mwaka 2020 peke yake watu milioni 275 walitumia mihadarati ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 22 kutoka mwaka 2010.
Ni ukweli kwamba matumizi ya dawa za kulevya ni tatizo sugu kutokana na mzizi hasa wa jambo lenyewe na namna ambavyo biashara hiyo inavyogusa maslahi ya watu mbalimbali, Kwa Tanzania pekee hadi kufika leo tumeshuhudia vifo vya idadi kubwa ya vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa, tena mbaya zaidi wengine walikuwa ni watu maarufu.
Licha ya kwamba utafiti wa UNODC ulifanyika zaidi kwa mataifa makubwa yenye idadi kubwa zaidi ya watu duniani lakini inaakisi ukweli na uhalisia wa hali ilivyo kwa vijana wanaojiingiza kwenye utumiaji wa Dawa hizi hatari za kulevya, kwa Mujibu wa Faraja yeye anasema ni Kundi la vijana wa Rika lake ndio chanzo halisi cha yeye kuanza kutumia Dawa hizo.
Kwa namna alivyodhoofika na dawa hizo Faraja ni mtu ambaye hawezi kukaa muda mrefu bila kupata Dawa zitakazomuondoa kwenye arosto, na hii ndio safari ya mazungumzo yangu mimi na yeye ilipoanzia.
Kituoni mwananyamala nikiwa nasubiria Gari Faraja alinifata na kuniita kwa jina ingawa mwanzoni alitanguliza neno Sister, nilipomtazama nilimtambua lakini hali yake ikanishangaza sana, hakuwa tena Yule Faraja niliyesoma nae Shule ya sekondari Toangoma.
Enzi za shule Faraja Alikuwa ni kijana mtanashati, mwenye upeo na maarifa makubwa sana, alikuwa anajipenda na hakuwa muongeaji sana na uso wake muda mwingi ulikuwa na aibu, Haya yote yalikuwa yanapita kichwani kwangu huku nikijizuia kabisa nisioneshe mshangao wangu mbele ya macho yake.
Nilimpokea kwa Tabasamu la uongo na kujidai namuuliza habari za siku nyingi, na baada ya mongezi yetu ya hapa na pale ndipo aliponigusia hitaji lake la shilingi elfu mbili, madai yake alikuwa na njaa anahitaji akale, hapa ndipo nilipopata ujasiri wa kumwambia kuwa nitampa hiyo pesa lakini endapo atanipa ushirikiano wa kunielezea kwanini yupo kwenye hali ile, Nilimuweka kwenye mtego huo kwa sababu nilijua wazi kuwa anataka pesa kwangu ili akatafute dawa aendelee kujidunga.
Faraja hakuwa na namna zaidi ya kukubali ombi langu, nikavunja ratiba yangu ya kupanda daladala nikamchukua tukatafute sehemu ili apate kunisimulia, na hii ndio safari ya Simulizi Y afaraja ilipoanzia.
“Mwanzo sikuwa najua kabisa kama rafiki zangu wanatumia hizi dawa, na hata nilipokuja kugundua sikuwa tayari kabisa kujiunga na” alielezea kwa hisia sana Faraja, kupitia maelezo yake nilibaini kuwa hata yeye mwenyewe hakuwa anayapenda yale maisha.
“Nilikuwa naamini kuwa naweza kuwa na urafiki nao bila ya mimi kutumia, na mara kadhaa nilikuwa nawaonya wasitumie lakini hawakuwa wananielewa, na muda mwengine waliniambia kuwa nijaribu tu hata siku moja ili nione raha wanayoipata”
Aliendelea kusema Faraja, na hadi kufikia hapa nilikuwa na swali moja tu ambalo lilikuwa kichwani mwangu,swali la kwanini sasa na yeye akawa miongoni mwao?? Swali hilo lilinifanya niendelee kuwa makini kumsikiliza Faraja.
“Bila ya kujua sister, nilipokuwa natoka nao kumbe walikuwa wananiwekea kwenye kinywaji changu, mwanzoni nilikuwa nahisi napata ‘vibe’ la tofauti sana nikigonga vitu vyangu, mpaka nilipokuja kushtuka tayari nilikuwa nalitamani lile ‘vibe’ niendelee kulipata siku zote”
Kifungo hicho cha maelezo ya Faraja ndicho kilichokuwa na majibu ya maswali yangu mazito ya jinsi gani aliingia kwenye ulimwengu huu wa mateso na kifo, kichwani yakarudi pia maelezo ya watu wengine waliokuwa wakitoa ushuhuda wao hadharani juu ya namna gani waliingia kwenye matumizi ya Dawa za Kulevya.
Ni ukweli kwamba wengi wao huingia katika jinamizi la matumizi ya dawa hizi za kulevya kwa ushawishi wa watu wao wakaribu, aidha wapenzi wao au marafiki zao, na wakati mwengine watu hao bila huruma huwaingiza wengine kwenye matumizi ya dawa hizo kwa hila za kuwachanganyia mara kwa mara.
Kuendelea kupigana vita kwa mtindo wa aina moja bila kubadili mbinu za mapigano ni jambo ambalo si jema katika mustakabali mzima wa ushindi wa kishujaa dhidi ya adui unayepigana nae, nadhani kuna haja sasa ya vita hii ya matumizi ya dawa za kulevya ihamie katika kuwanusuru watu ambao wanaingizwa kwa wingi na watu wao wa karibu. Watu kama Faraja ndio silaha ya kuizindua jamii yetu hasa vijana ambao huenda wanaona kuwa wapo salama wanapofika bara na marafiki zao kumbe ndio chanzo cha wao kuangamia kwa kuwekewa vitu hivyo kwa siri.
Ni vema kukafanyika tafiti za kutosha ili kuona idadi ya vijana wanaoingia kwenye matumizi ya dawa hizi kwa mtindo huu ni ngapi na pia kutafuta njia ya kutoa elimu kwa watu juu ya namna gani wajilinde wanapokuwa na watu wao hasa wanaowaamini, hii inaweza isisaidie kutokomeza matumizi ya dawa za kulevya kwenye jamii yetu lakini kwa hakika inaweza kupunguza idadi ya wanaoingizwa kwenye matumizi haya bila ya hiyari yao na hii itaathiri pia ongezeko la kasi la watumiaji wa dawa za kulevya duniani.
Tafiti zinaonesha kuwa ongezeko la watumiaji dawa za kulevya ni asilimia 30 ukilinganisha na miaka 10 iliyopita ikihusisha bara letu la afrika, Asia, Ulaya na Amerika Kaskazini kwa Tanzania ongezeko hilo limechangiwa pia na Faraja ambaye masikini yeye ameingia katika ulimwengu huo bila yakupenda.
Badala tu ya kulaani wanaofanya biashara hiyo ifike mahali tufanye kwa vitendo kwa kuwachukua vijana kama Faraja na kuhakikisha wanapona ili muwape ajira katika taasisi za ndani zinazojihusisha na mapambano dhidi ya dawa za kulevya, nina uhakika watakuwa mabalozi wazuri wa kudhibiti mwanya wa wanaoingizwa kwenye dawa hizi kwa hila za watu wao wa karibu.
Nisiwachoshe wakuu acha nikamilishe na pigo la kuondokewa na Faraja September 17 mwaka jana, kijana mwezetu wa Kitanzania alifariki Dunia, amezikwa nyumbani kwao Morogoro na chanzo halisi cha kifo chake ni hizo hizo dawa za kulevya.
Kama mmoja wa watu ambaye nilisoma na faraja na kubahatika kupata simulizi yake ambayo alinisimulia mwenyewe niliguswa na kifo cha kijana mwenzangu na maumivu ya kuondokewa na aina ya kifo alichokufa nacho yeye bila shaka kinawakuta wazazi na watu wengine wa karibu wa vijana wenzetu wa kitanzania wanaotumia dawa za kulevya kila siku iitwayo leo.
Andiko langu likawe Baraka na kuwakumbusha wenye mamlaka ya kwamba Nguvu kazi inamalizwa na dawa za kulevya, Vita hii inahitaji ubunifu na weledi wa kupambana na sio nguvu wala sifa za maneno matupu ya kutafuta umaarufu wa kisiasa.

Upvote
3