Wabongo bana!!!

FourTwoNet

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2022
Posts
1,236
Reaction score
2,512
Yani huku bongo, mwenzetu akijaribu kujiachia na lugha ya kigeni, watatokea maprofesa wa lugha kila kona....

"Ooh! Kingereza feki..." ....."Apo kabomoa"....mara "Anajifanya"....mara "Huyu, anatuaibisha"....

Maprofesa wenyewe unakuta ushamba tu, hakuna anayejua hili wala lile...akishajua kusema anaitwa nani kwa kilami baaaaas, yeeh gwiji! Wanaojua kiingereza chenyewe kweli, hautawakuta wakicheka, sana sana watamani jamaa aendelee mwendo huo huo, ipo siku kitakaa vizuri.

Wenzetu hapo Kenya, Uganda na sekta kama Rwanda...huwa hawachekani, na vingereza vyao huwa vimeathiriwa na lugha zao za mama vibaya mno...lakini huwa sio ishu kwao kwenye mambo ya msingi....na ikitokea wanachekana, ni fasihi, kwenye vichekesho...lakini huwa hawaumbuani.

Njoo hapa bongo sasa....ushamba mtupu. Yani "crabs in the barrel mentality"...kwa kifupi ni kama vile mvuvi sio lazma aweke nyavu kwenye ndoo aliyojaza kaa, maanake mmoja akikaribia kufika juu, hao waliopo chini wanamvuta asiende mahali.

Tuache upuuzi tafadhali...wivu unaua!!! Binafsi mi sio mtu wa WCB na wala sifagilii uswahili wao, ila mgala muue na haki yake umpe. Mondi anajitahidi na inatakiwa apewe "sapota" kwenye swala zima la kimombo.

Kina Harmo pia wanajitahidi sana tu..

Tusipende kupeana aibu kwenye swala la maendeleo. Au mnasemaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…