Wabongo sina hamu nao

barakachaplin

Senior Member
Joined
Jan 24, 2014
Posts
118
Reaction score
53
Watu kweli wamezoea vya kunyonga!!!!....
WABONGO SINA HAMU NAO...!!
Jamaa alinunua friji jipya, akawaza namna ya
kuondokana na lile la zamani, basi akaliweka
nje ya nyumba yake na kuandika kibao:-
"ANAYE TAKA KUCHUKUA, ACHUKUE BURE".
Watu wakawa wanapita wanafungua lakini kila
mtu akawa anaogopa kuchukua maana hakuna
aliyeamini mtu anaweza akagawa friji zima
bure.
Baada ya kuona wiki imepita halijachukuliwa,
akaandika:-
"FRIJI INAUZWA LAKI 3"
Usiku uleule likaibiwa...
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] mbavu zangu
 


Usitake ncheke, inaonekana mkuu unakaa uswahilini sana. Mpaka unauza na friji!!? kweli nimekubali kutumbuliwa kuna athari kubwa.
 
ndio hivyo hata majambazi wakikuta mlango uko wazi hawaingii... wanasubiri ufungwe wauvunje ndo waingie.
 
ndio hivyo hata majambazi wakikuta mlango uko wazi hawaingii... wanasubiri ufungwe wauvunje ndo waingie.
Ni kweli hata mi mwenyew nikitaka kudokoa kitu siwez dokoa kilichowaz bali kilichofichwa ndo chenyew haswaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…