Wauzaji kama hawa hata VETA hawafaiJana kuna sehemu nimeenda, nikakuta ndala zile kandambili za 2000 zinauzwa 5000, kuuliza haipungui nkaambiwa haipungui alafu muuzaji akaendelea kujisnap.
Mjini shule mkuu ukiwa unateseka na vyakusikia na kuona utaishi maisha ya shida sana.Na hizi stori za mitandaoni kila mtu amataka kitusua maisha ni balaa.
Stori za Madalali
Dalali 1: Juma amepiga hela san, Baba ́Mwenye nyumba kataka milioni 50, aisee Juma si akapata mteja wa mil 110? Juma kapiga milioni 60 cha juu.
Dalali 2: Mjini mipango akija fala unapiga tu, ile prado naifanyia mpango Sitakosa hata 10M hivi.
Mambo yako hivyo kwenye biashara zote.
Mwenye nyumba kasema anapangisha kwa laki 2, Dalali Juma anakupiga laki tatu 50.
Mtu kanunua Kuku elfu 7, anakupiga elfu 18😅😅😅
Acheni mpigwe tu kwasababu hela mnatapanya kwa michepuko badala yakuungisha watanzania wenzenu.Leo nimeiona hii
Nimeenda dukani kununua dawa ya mswaki whitedent yenye uzito wa 70 g.
Duka la kwanza bei nikatajiwa 1,500 Tsh
Duka la pili bei nikatajiwa 1,700 Tsh
Duka la tatu bei nikatajiwa 2,000 Tsh
Swali nikajiuliza kwa nini bei iwe tofati wakati mtengenezaji ni yule yule na nipo ndani ya mtaa huo huo?
Kwa kweli wateja tunaibiwa sana. Tatizo hili litakomeshwa kwa kila bidhaa atakama ni pipi ya Tsh 50 iandikwe bei