Wabunge 11 wafanya ziara ya siri nchini Somalia. Wahusishwa na matukio ya ugaidi huku uchunguzi zaidi ukiendelea dhidi yao

Wabunge 11 wafanya ziara ya siri nchini Somalia. Wahusishwa na matukio ya ugaidi huku uchunguzi zaidi ukiendelea dhidi yao

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
WABUNGE 11 kutoka eneo la Kaskazini Mashariki mwa Kenya, Jumapili walinaswa na polisi mara tu baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), Nairobi kutoka Somalia.

Wabunge hao walielekea nchini Somalia bila idhini kutoka kwa Wizara ya Masuala ya Kigeni wala Spika wa Bunge Justin Muturi inavyohitajika kisheria, kulingana na duru za Idara ya Kuchunguza Uhalifu (DCI).

Kwa msingi huo, safari yao iliibua maswali miongoni mwa asasi za kiusalama nchini humu kuhusu nia yao kwa kiwango cha serikali kuhusisha kitengo cha kupambana na ugaidi kuwanasa walipowasili.

Walikuwa wameelekea Mogadishu Jumamosi na ripoti zinadai walikutana na maafisa wa ngazi ya juu wa idara ya usalama nchini Somalia, madai ambayo yamewafanya maafisa wa upelelezi wa humu nchini kutaka kujua kile walichoenda huko kujadili.

Wabunge hao ni Adan Ali sheikh (Mandera Kusini), Mohamed Dahir (Dadaab), Ahmed Bashane (Tarbaj), Kullow Maalim (Banisa), Ahmed Kolosh (Wajir Magharibi), Ibrahim Abdi (Lafey), Rashid Kassim (Wajir Mashariki), Mohamed Hire (Lagdera), Omar Maalim (Mandera Mashariki), Bashir Abdullahi (Mandera Kaskazini) na Adan Haji (Mandera Magharibi).

Sita kati yao wanatoka Kaunti ya Mandera, watatu kutoka Wajir na wawili wanatoka Garissa.

Waliabiri ndege ya Salaamair Air Express Flight WU-751 hadi mjini Mogadishu, Somalia. Hata hivyo, Katibu wa Usalama wa Ndani Moffat Kangi alisema waliachiliwa huru baada ya kuhojiwa, na hawatashtakiwa.

Maafisa wa polisi Jumapili walikuwa wamekita kambi katika JKIA na uwanja wa ndege wa Wilson tangu asubuhi wakiwangoja kuwanasa wabunge hao.

Usalama uliimarishwa huku polisi wakipiga doria kila lango kuhakikisha kuwa wabunge hao hawatoroki.

Magari ya Polisi wa Kupambana na Ugaidi Jumapili yalionekana yakizunguka kati ya uwanja wa JKIA na Wilson.

Kamanda wa Polisi wa Kituo cha JKIA Titus Ndungu alisema waliimarisha doria katika viwanja vya JKIA na Wilson kwa sababu hawakuwa na taarifa kuhusu ndege ambayo wabunge hao wangetumia kurejea humu nchini.

Walipowasili Kenya, maafisa wa uchunguzi walitaka kujua lengo lao kusafiri katika nchi ya kigeni bila idhini ya serikali ya Kenya.

Ripoti zinadai serikali ya Somalia inawatumia kushawishi Kenya kukoma kuunga mkono viongozi wa Jubaland – ‘nchi’ ambayo haitambuliwi na Umoja wa Mataifa – wakiongozwa na Ahmed Mohamed Islam Madobe.
 
Actually Farmaajo plans to 'EXPEL' KDF from Somalia. - Somali politicians to ENGINEER anti-KDF 'demonstrations' in ex-NEP & call for KDF withdrawal while denouncing AMISOM.
 
Huko kuna Mh Kangi? Safi sana Kangi wa kenya
 
Hakuna siri yeyote chini ya jua ambayo huwa inadumu kwa muda mrefu. Huu ndio mwanzo wa mwisho kwao, hawa dawa yao ni ATPU. Hata akina 'Sheikh' Aboud Rogo, nduguye 'Sheikh' Ibrahim Rogo na Sheikh mwenzao feki Makaburi walitamba sana enzi zao. Ila sasa hivi hata mazombie wafia dini, ambao walikuwa wanawashabikia sana enzi hizo, huwa hawawakumbuki hata kwa maombi.
 
Hakuna siri yeyote chini ya jua ambayo huwa inadumu kwa muda mrefu. Huu ndio mwanzo wa mwisho kwao, hawa dawa yao ni ATPU. Hata akina 'Sheikh' Aboud Rogo, nduguye 'Sheikh' Ibrahim Rogo na Sheikh mwenzao feki Makaburi walitamba sana enzi zao. Ila sasa hivi hata mazombie wafia dini, ambao walikuwa wanawashabikia sana enzi hizo, huwa hawawakumbuki hata kwa maombi.
Haha!🤣🤣 Imeandikwa kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe...
 
Haha!Imeandikwa kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe...
Exactly ndugu yangu! Hakuna mtu yeyote ambaye ana haki ya kumuamulia binadamu mwenzake siku zake za kuishi hapa duniani. Tena binadamu wasiokuwa na hatia na ambao hawajamdhulumu mtu yeyote yule. Malipo ni hapa hapa duniani. Live and let live. Makaburi alikuwa anasema live misikitini kwamba dawa ya kafiri ni bunduki. Kwa upumbavu wake leo hii watoto wake hawanana baba, na mke wake naye najua kwa uhakika kwamba ameshahamia kwa jemba mwingine. Yote kwasababu ya hiyo hiyo bunduki. Waliomsifia hadi akavimba kichwa bado wanaenjoy maisha na hakuna mmoja wao anayemkumbuka, isipokuwa hater wake pingli-nywee. 😁
 
Mpaka Sasa walio comment wamekurupuka na mbumbumbu kweli JF imevamiwa ukisoma Uzi utaona inasemekani serekali ya Somalia inawatumia hao wabunge kuishawishi serekali ya Kenya isiwaunge mkono Jimbo la jubaland linalotaka kujitenga mbumbumbu wamekurupuka wanaleta udini shwain

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka Sasa walio comment wamekurupuka na mbumbumbu kweli JF imevamiwa ukisoma Uzi utaona inasemekani serekali ya Somalia inawatumia hao wabunge kuishawishi serekali ya Kenya isiwaunge mkono Jimbo la jubaland linalotaka kujitenga mbumbumbu wamekurupuka wanaleta udini shwain

Sent using Jamii Forums mobile app
Tena na wengine wanaonekana wanamalizia hasira zao za shida zao kwa roho ya chuki kubwa kuliko
 
Back
Top Bottom