Wabunge CCM wamlilia Tundu Lissu awe waziri wa Katiba na Sheria nchini

Wabunge CCM wamlilia Tundu Lissu awe waziri wa Katiba na Sheria nchini

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,925
SAMWEL SITA NA TUNDU LISSU.JPG

Wajumbe wawili wa Bunge Maalum la Katiba, ambao ni wabunge wa CCM, Abdul Marombwa (Kibiti) na Christopher Ole Sendeka (Simanjiro) kwa nyakati tofauti wamempongeza Tundu Lissu, kwa kujibu maswali na kutoa ufafanuzi mzuri wa masuala ya kanuni kama vile waziri.

Lissu Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki (Chadema) na sasa ni Mjumbe wa Kamati ya Kumshauri Mwenyekiti wa Muda kuhusu Rasimu ya Kanuni za Bunge hilo, aliwakosha wajumbe wengine kwa kujibu maswali ya wajumbe kuhusu sheria na kanuni kwa uelewa mkubwa.

Ole Sendeka alitoa pongezi zake bungeni juzi jioni wakati wabunge wakiendelea na semina yao kuhusu Rasimu ya Kanuni za Bunge Maalum. “Kwanza nakupa pongezi sana kwa umahiri wako wa kujibu na kutoa ufafanuzi wa maswali mbalimbali ya kisheria na kanuni, ningependekeza mheshimiwa rais angekuteua kuwa Waziri wa Katiba na Sheria,” alisema.

Marombwa alimpongeza Lissu wakati akizungumza na NIPASHE nje ya ukumbi wa bunge siku mbili kabla ya Sendeka kufanya hivyo.
“Amekuwa akijibu maswali ya wajumbe bila kuonyesha upendeleo au misimamo ya chama chake. “Anajibu na kutoa ufafanuzi mzuri kama vile waziri, mara zote haonyeshi kuegemea upande wa chama chake kama inavyokuwa wakati wa mijadala ya Bunge la kawaida,” alisema.

Moja ya hoja ambazo Lissu alizitolea ufafanuzi ni hoja ya kuwa na ‘mgeni rasmi’ ambayo katika tafsiri ya Rasimu ya Kanuni hiyo imesema ni Rais wa Jamhuri ya Muungano au Rais wa Zanzibar atakayealikwa na Mwenyekiti kulihutubia Bunge Maalum. Akizungumzia matarajio yake katika Bunge Maalum la Katiba, alisema wanaweza kuipata Rasimu inatakayopendekezwa kama wajumbe wataondoa tofauti na itikadi za kivyama.
 
Ila wakumbeke yapo Albet msando lisu akimwona anajificha
 
Hii siyo habari itakayoaminiwa ama kuungwa mkono na wana LUMUMBA, subiri uone watakavyouchafua huu ukurasa.
 
Lissu akisimama kutoa hoja bungeni zinazohusu sheria basi mwanasheria wetu mkuu huwa hana amani kabisa!!
 
CHADEMA mnapenda sifa za kitoto, kuna kipindi tena mlizusha kuwa Jakaya Kikwete anamuogopa Tundu Lissu.
 
Ni kweli kama wajumbe wa ccm wataacha ushabiki basi hakuna shaka tutapata katiba nzuri kwa rasimu iliyopo
 
alibet sando wakili wa zitto huwezi kumlinganisha na tundu lisu. tundu lisu ni kiboko ya mawakili wote hakuna wakumfikia hata mmoja. chunguza kama yopo, tuambie ninani.
 
Ila pia mkumbuke anazichanga wakati mwingine na kuwachanganya wenzake
 
Kwani Jakaya kwenye kampeni za mwaka 2010 aliposema "...Afadhari Dr Slaa awe raisi kuliko Tundu Lissu kuwa mbunge.." Hii maana yake ilikuwa ni nini?!
Alisemea haya maneno wapi? Mbona Tundu kawa Mbunge na Dr.Slaa sio Rais..na bado JK ana-survive? Acheni uongo nyie BAVICHA.
 
Alisemea haya maneno wapi? Mbona Tundu kawa Mbunge na Dr.Slaa sio Rais..na bado JK ana-survive? Acheni uongo nyie BAVICHA.

Ungekuwa makini usinge stahili kuniuliza hayo maswali. Ulipaswa kumuuliza yeye kuwa kule Singida alipo sema maneno hayo alikuwa ana maanisha nini?
 
Ungekuwa makini usinge stahili kuniuliza hayo maswali. Ulipaswa kumuuliza yeye kuwa kule Singida alipo sema maneno hayo alikuwa ana maanisha nini?
Kwa faida ya akina sisi ambao hatukusikia hayo maneno yakitoka kinywani mwa Rais wetu, labda ungetuwekea video clip au Audio clip tumsikie rais.
 
Kwa faida ya akina sisi ambao hatukusikia hayo maneno yakitoka kinywani mwa Rais wetu, labda ungetuwekea video clip au Audio clip tumsikie rais.

Mkuu wala usipate tabu, wewe waulize wenzako hapo Lumumba wanajua na huenda wanazo clip mimi sinazo bali ni kauli ambayo nitaendelea kuikumbuka maana hata Lissu alipotaka kuvuliwa ubunge kwa hila nukuu hiyo ilirejelewa mahakama kuu kanda ya kati pale Dodoma na bado Lissu akashinda ile kesi. Sijui unakumbuka?!
 
Back
Top Bottom