Wabunge katiba, mungu hawapendi mafisadi.

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
1,985
Reaction score
1,286
"Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo." Yuda 1:4

"Na utafute, kwa aliyo kupa Mwenyezi Mungu, makaazi ya Akhera. Wala usisahau fungu lako la dunia. Nawe fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyo kufanyia wema wewe. Wala usitafute kufanya ufisadi katika ardhi. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi mafisadi."
Qur-an 28:77

Wabunge wa bunge la katiba kufanya kazi zao huku wakiongozwa na matakwa yao badala ya matakwa ya watu waliowatuma na mbaya zaidi kutumia muda vibaya ni matumizi mabaya ya fedha za umma. Mfano muda waliotumia kwajili ya kujadili posho ungeweza kutumika kujadili mambo ya msingi kuhusiana na katiba tunayoindika. Wanajua fika, kila siku moja ya wao kuwa Dodoma mamilioni ya fedha za umma hutumika, lakini bado wanafanya utoto badala ya kazi iliyowapeleka.

Hivi kwa kazi iliyo mbele yao wanapata kweli muda wa kufikiria kuiba simu na laptop? Wabunge wetu ni vema wajue kuwa MUNGU hapendi ufisadi na wafanyao ufisadi, haijalishi huyo mungu ni NG'OMBE au KINJETILE.


Njano5.
0784845394.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…