Wabunge Kenya wamekwenda kuangalia kombe la dunia kwa gharama ya nani?

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Wakenya wamekasirishwa na taarifa kwamba wabunge 20 wamesafiri kwenda Urusi kutazama kombe la dunia kwa gharama ya fedha za umma.

Wamekwenda kutazama mechi nne, ikiwemo fainali kati ya Ufaransa na Croatia, katika safari ya wiki mbili inayokadiriwa kuwa na thamani ya maelfu ya dola.

Mjadala ulizuka baada ya wabunge hao kuweka picha walizopiga uwanjani.

Waziri wa michezo Rashid Echesa ameiambia BBC kwamba alitoa idhini kwa wabunge 6 pekee kusaifiri, kusaidia kuelewa jinsi matukio makubwa ya kimataifa yanavyoandaliwa.

Kenya haijawahi kufuzu kwa fainali ya Kombe la Dunia na imeorodheswha nafasi ya 122 kati ya matifa 206 na shirikisho la soka duniani FIFA.

Hatahivyo Kenya ina umaarufu mkubwa katika riadha na ni mojawapo wa mataifa yenye ufanisi mkubwa duniani .

Tayari nchi hiyo imewasilisha ombi la kutaka kuwa mwenyeji mashindano ya kimataifa ya riadha mwaka 2023.

Lakini hisia iliopo kwa Wakenya ni kwamba safari hiyo ni upotezaji wa fedha za umma katika nchi ambayo kipato cha mtu wa kawaida ni $150 kwa mwezi.

Katika maoni yaliopo huyu anastaajabishwa na hatua hiyo akieleza kwamba huwezi kuwaona viongozi wakitazama hata mechi za ndan ya nchi kuinusha talanata ya ndani lakini wabunge wana muda wa kujigamba kwa picha Urusi.
 


Kuna kitabu nilisoma cha Mkenya kinaitwa ,,its our turn to eat” majibu yote yamo humo kwenye hicho kitabu kuhusu hiyo nchi na watu wake, kwa kifupi ni dog eat dog society.

Asante Mungu kwa kutuletea Raisi Magufuli TZ yetu, huo ujinga hauwezekani kutokea TZ chini ya Raisi wetu Magufuli.

Angalau ningeelewa kama timu ya Kenya ingekuwa inacheza lkn Croatia na Kenya wapi na wapi?
 
Wameenda kujifunza.miafrica letu moja.
 
Korosho zimewashinda ya Your Big Brother Kenya mtaweza?
 
Mafao ya waliostaafu meshindwa kulipa Yani ushamba mwingine bhana bila kusahau korosho na na ile 1.5 trillion na pia SGR kusimama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…