Wabunge Kenya waomba Usalama wa Rais kuimarishwa na kuongezwa ulinzi kwa Wabunge zaidi ya 290 waliounga mkono hoja ya kuondolewa Naibu wa Rais Kenya

Wabunge Kenya waomba Usalama wa Rais kuimarishwa na kuongezwa ulinzi kwa Wabunge zaidi ya 290 waliounga mkono hoja ya kuondolewa Naibu wa Rais Kenya

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Hayo yameelezwa na wabunge baada ya hoja maalumu ya kumbandua naibu wa Rigathi Gachagua kuwasilishwa bungeni mchana wa leo Oct 01.2024.

Kiongoza wa wachache bungeni Mh.Junet Mohamed alitoa angalizo la kiusalama mbele ya spika na kwamba Inspekta Generali mpya wa polisi anawajibika kuwahakikisha ulinzi na usalama wa wabunge haswa waliotajwa kwa majina bungeni, kulingana na unyeti na uzito wa hoja yenyewe. Mh.Juneti aliongeza kwa kutoa wito kwa wabunge hao wote waliotia sahihi muswada huo, siku ya kutoa uamuzi wa mwisho asikosekane hata moja, wote wawepo.

- Hoja maalumu ya kumwodoa Gachagua yawasilishwa bungeni

Kwa upande wake Mh.Maalim Farah mbunge wa Dadaab, alidai haitoshi tu kuwalinda wabunge 291 waliosaini kuunga mkono muswada huo, bali pia ni Lazima kuulinda mfumo wa kiusalama na Inspector Generali wa polisi ni muhimu kumlinda RAIS kufa na kupona, akiwakumbusha aina ya katiba walio nayo kwamba any reckless thugs can decide to change the course of history.

Hayo yote yamekuja baada ya uvumi uliosambaa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii Kenya kwamba kabla ya March 2025, bendera inaweza kua inapepea nusu mlingoti.

Kiongoza wa wengi bungeni Kimani Ingung'wa, aliwahakikishia wabunge hao usalama wa uhakika, na alimueleza spika kwamba analazimika kumulekeza Inspekta Generali mpya wa Polisi, ambae alithibitishwa na bunge hilo chini ya mwezi moja uliopita, kuhakikisha kwamba wabunge wanakua salama kwenye kazi za kamati, ndani na nje ya bunge na mpka majumbani mwao na hasa ukizingatia wakati huu ambapo, alisema we are not dealing with an ordinary matter, we are not dealing with an ordinary man, we are dealing with black man with black heart. Alihitimisha hivyo Kimani Ingung'wa kiongozi wa wengi bungeni.

Je, kwanini wabunge wamejawa hofu hasa wanapojadili hoja hii ya kikatiba ya kumbandua naibu wa rais Rigathi Gachagua? Ni kwa kiasi gani anatisha mtu huyu hata wabunge waingiwe kiwewe hivyo 🐒

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Acha waendelee kuvurugana sana ,huku sisi watanzania tukiendelea kujenga uchumi wetu chini ya Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.
 
Actualy si mbovu. Moja ya katiba ambazo inalazimika uwajibikaji wa viongozi to the max.

Imetengenisha chama na serikali kiasi kwamba chama hakiwezi kutumia vyombo vya serikali kujinufaisha bila muhimilu wa sheria kuwakamata
chama bado nguvu yake ni kubwa mno, na ndiyo maana wateuliwa wote wa chama huthibitishwa na bunge kirahisi sana, na hata wale wanaokua endorsed na chama kuomba nafasi za uongozi mbele ya tume au jopo maalumu la kuwathibitisha kirahisi, na kisha rais kuwateua alikokusudia.

hata huu mudwasa wa kumbandua gachagua, umeanzia kwenye chama tawala na katibu mkuu wa UDA Hassan Omar alithibitisha hilo.:pulpTRAVOLTA:

Kwa nini wanambandua?
Yes,
Hoja maalumu ya kumbandua kwenye wadhifa wake wa unaibu wa rais imewasilishwa tayari leo hii bungeni.
Zipo tuhuma zaidi ya 8 za kikatiba, kisheria na kimaadili zinazomkabili :pulpTRAVOLTA:
 
chama bado nguvu yake ni kubwa mno, na ndiyo maana wateuliwa wote wa chama huthibitishwa na bunge kirahisi sana, na hata wale wanaokua endorsed na chama kuomba nafasi za uongozi mbele ya tume au jopo maalumu la kuwathibitisha kirahisi, na kisha rais kuwateua alikokusudia.

hata huu mudwasa wa kumbandua gachagua, umeanzia kwenye chama tawala na katibu mkuu wa UDA Hassan Omar alithibitisha hilo.:pulpTRAVOLTA:

GACHAGUA the sixth
 
Chama hakina nguvu kama zamani. Kabla kibaki hajaingia madarakani, chama kikuu kilikuwa similar to ccm, kina uwezo wa kuhodhi vyombo vya dola kwa kazi zao, wanaweza kutumia rasilimali za serikali vile wanavyoona.
Kibaki alipo badili katiba na kila kitu kikabadilika

Angalia tu mawaziri, ma jaji wa mahakama wanapatikanaje. Ile influence na lobying za kichama zimeondolewa. Hata kama zipo hazina nguvu tena. Wamefanikiwa kutenga shughuli za serikal na chama
 
kwamba judge au maafisa wowote wa kupitia tume ya ajira, kuthibitishwa na Bunge na kisha ateuliwe na Rais apite huko kote bila endorsement ya chama cha UDA?🤣

Thubutu! si itakua fujo sasa huko serikalini gentleman 🐒
 
Ruto naye ni mwenyekiti wa chama tawala cha Kenya kama kule Kwa yule bibi?
Ruto ni Party leader wa United Democratic Alliance UDA, na kinara wa muungano wa KENYA KWANZA wenye vyama vya siasa zaidi ya 10🐒
 
Back
Top Bottom