Wabunge kulipa ada

Mnyampaa

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2011
Posts
244
Reaction score
58
Wana JF nifungueni katika hili. Wabunge kulipia ada wanafunzi ni PUBLIC RESPONSIBILITY ya mbunge au ni RUSHWA kwa wapiga kura. Ninaelewa kuna mfuko wa kusomesha wasiojiweza katika Halmashauri ingawa sifahamu unavyoendeshwa. Kwa hili naona lina utata. Kama ni sehemu ya wajibu, na wazazi wafanye nini?
 
Kila kitu kina utaratibu wake, mifuko ipo na matumizi yana utaratibu wake.
Kuna mifuko mingine mingi tu ukiacha hiyo ya kusomesha watoto.
Mbunge kutoa pesa mfukoni mwake na kulipia ada watoto sioni kama kuna ubaya. Anaweza kuwa ni mbunge wa mahala fulani lakini hajapewa fungu litakalosaidia mambo ya kielimu kwa kipindi hicho au fungu limechelewa, inawezekana watoto wamemlilia shida hvyo kwa huruma yake anatoa pesa mfukoni. Kuna mbunge flani wa singida alikuwa anasaidia sana watoto kwenye mambo ya shule tena kwa pesa yake binafsi.
Mungu awazidishie wabunge wote wa namna hyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…