Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
KWA UFUPI
Kutokana na kazi kushindwa kufanyika kwa wakati hasa kutokana na zuio la wananchi mahakamani.
Dar es Salaam. Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu wanakusudia kupeleka muswada kuomba marekebisho ya Sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999, wakidai inasababisha wananchi kulipwa fidia kidogo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Peter Serukamba alisema sheria hiyo inayohusu fidia kwa wananchi wanaohamishwa makazi yao kupisha utekelezaji wa ujenzi miundombinu na majengo mbalimbali, imekuwa ikiwakandamiza wananchi kulipwa kidogo tofauti na gharama halisi.
Ni gharama kubwa kwa Serikali inapotokea wananchi wamegomea fidia, wakati huo tayari mkandarasi yupo eneo la ujenzi unakuta fedha zinatolewa kulipa riba ya mkandarasi, alisema Serukamba na kuongeza:
Kutokana na kazi kushindwa kufanyika kwa wakati hasa kutokana na zuio la wananchi mahakamani.
Kamati hiyo juzi ilikubaliana kupeleka muswada wa kufanya marekebisho sheria ya ardhi, ilipofanya ziara ya kukagua miundombinu mbalimbali, ikiwamo daraja linalojengwa juu ya bahari kati ya Kigamboni na Kurasini.
Licha ya changamoto nyingine, wananchi waliogoma kuhama kutokana na fidia kidogo ambayo haiendani na hali halisi.
Mbunge wa Viti Maalumu, Zarina Madabida alitaka kujua sababu za Serikali kulipa fidia kidogo kwa wananchi wanaotakiwa kupisha ujenzi wa miundombinu, hali hiyo inayosababisha manunguniko.
Pia, walionyesha kukerwa na msongamano wa magari Dar es Salaam kwamba inapaswa kudhibitiwa kabla haijaambukiza majiji.http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/1597578/1727202/-/w1uogu/-/index.html