kibaravumba
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 6,634
- 7,015
Tunajua sasa suala la posho ilikuwa mpango mahsusi wa wasiolitakia mema taifa kututoa kwenye mjadala wa msingi ambapo sasa ni kanuni za kuendesha bunge maalum la katiba.Sisi wananchi wa Tanzania,tuliokubali muwe wawakilishi wetu huko Bungeni,tunataka kujua kanuni hizo zikoje kabla hamjazijadili,ili tutoe maoni yetu ikiwa ni kuboresha na kuweka wazi kila hatua ili mjadala uwe na baraka zote.Tunasikia tu kuna njama za kutaka kuweka ukiritimba na kufanya mambo mengine kama siri.Tusingependa mambo haya yatokee na kulazimisha njia za mashinikizo ambazo mara nyingi hugharimu muda na hata maisha ya watu.Mungu ibariki Tanzania
Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums