Wabunge maroboti

Wabunge maroboti

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Wajumbe wa bunge la katiba mlioko Dodoma usiwe kama maroboti yanayopangiwa na mtengenezaji nini cha kutenda bila kufikiri hata kidogo. Sisi wananchi tunafahamu na tunafuatilia yanayotendeka huko mjengoni kuhusu mjadala wa katiba, hivyo tunajua ni wajumbe gani wako kama maroboti yaliyoamriwa cha kufikiri na kutenda ndani ya bunge. Maana hata Nyerere alisemaga kuwa kama mtu mwenye akili timamu atapewa usharauri wa kijinga na mtu mwenye akili timamu halafu akaukubali na kuutekeleza kama ulivyo, basi mtoa ushauri atakuwa anamfanya mjinga mpokea ushauri huo.
Hivi mjumbe wa bunge la katiba mwenye akili timamu utakubalije kupewa ushauri/msimano wa kijinga na mtu mwingine mwenye akili timamu kama wewe na kuukubali?

Jiulize mwenyewe maswali yafuatayo:
1. Ushauri/msimamo unaopewa una maslahi gani kwa watu wa Tanganyika na Zanzibar?
2. Katiba tuliyonayo ilitungwa na wakina nani? na walikuwa wangapi?
3. Rasimu ya katiba mpya imetungwa na wakina nani? na walikuwa wangapi?
4. Kura ya wazi au kura ya siri zitasababisha matokeo gani ndani ya jamii? amani, chuki, upendo, mshikamano uadui uwadui kati ya mtu na mtu?
5. Wewe unadhani watanzania (bara na visiwani) wanataka katiba ya namna gani? na kama wasipoipata katiba wanayoitaka kwasababu yako na ujanja ujanja unadhani matokeo yake kwa miaka 50 mingine ijayo yatakuwaje? manung'uniko, furaha, kupendana, kuchukiana, uchumi kukua, uchumi kudorora, ugaidi, utulivu au nini? taja ___

Kuna wajumbe hapo wako kama maroboti leo hii mwenyekiti wa kundi lao akigeuka na akisema fanya hivi atafanya hivyohivyo bila kuhoji kama ndondocha.

Kwani shida yenu hasa maroboti ni nini? madaraka, woga, mali, heshima, kufa, kunyang'anywa au nini? taja_____

Fanya kazi kama wewe ili nchi iwe kama vile unavyotaka iwe
 
Ccm wanaamini bila ccm hakuna tanzania, huu ni upofu wa kifikra, shame on them!
 
Eee Mungu wa mbingu na nchi naomba jicho lako liangalie Dodoma na Sikio lako lielekeze hapo kwenye Bunge la Katiba,tazama kuna watu wanataka kutuharibia kuandikwa katiba itakayo tufaa sisi Watanzania tuliopo sasa na vizazi vijavyo kwa maslahi yao wenyewe ,sasa ukamhukumu kila atakaye tenda uovu huu na hukumu hii ikadumu mpaka kizazi cha nne cha uzao wake,siku zao zikawe chache,upanga,ukiwa na uharibifu vikawaandame usiku na mchana.

Kwa vile wamejitukuza sana wanaona wao ndo kila kitu eeeh Bwana kumbuka ulichomtendea Mfalme Nebukadreza mpaka alipokiri aliye juu ndiye anaye miliki na kutawala,mkono wako ukaunyoshee juu yao na familia zao mpaka watakapo jua wao ni wanadamu tu tena ni mavumbi na wewe ubaki kuheshimiwa mbinguni na duniani tena mkono wako ulionyooshwa mwanadamu hawezi kuurudisha nyuma,na atakayetoa wazo lake katika kuharibu mchakato huu hapo bungeni ahesabiwa sawa na yule aigusaye mboni ya jicho lako eeh Bwana na kuwa amesimama kinyume ya kila neno lililo jema mabaya yasiondoke hemani mwake siku zote za maisha yake ya kuishi duniani.
 
Back
Top Bottom