Benki ya Azania bank plc kwa mara nyingine imedhamini Bonanza la Wabunge wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania litakalowakutanisha wabunge mashabiki wa timu za Simba na Yanga litakalofanyika jumamosi hii katika viwanja vya shule ya John Merlini, Dodoma.
Leo hii Benki ya Azania imekabidhi vifaa kwa ajili ya Bonanza hilo,hafla ya makabidhiano hayo imefanyika Bungeni na kuhudhuriwa na viongozi na mashabiki wa timu hizo mbili kubwa.