Wabunge mnatia aibu, mmeligeuza bunge maalum kama soko

Wabunge mnatia aibu, mmeligeuza bunge maalum kama soko

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Ina sikitisha sana kuona wabunge wetu pamoja na wale wateuliwa wamemua kuligeuza bunge hili maalum kama soko.
Kwakweli yeyote aliyepata nafasi ya kutazama hata kidogo mjadala wa bunge maalum atakubaliana nami kuwa wabunge wetu wameligeuza bunge hili maalum kama soko ndio maana bunge hili limekuwa sehemu ya kelele, uropokaji na kuzunguka zunguka kama sokoni.

Wengi tulitegemea bunge hili maalum lingekuwa la utulivu na kusikilizana na wabunge wetu wangetumia hekima na busara zaidi katika mijadala yote, lakini kinyume chake tuna shuhudia watu kuropoka, kuzunguka zunguka bungeni,kupiga kelele wakati wengine wakichangia. Kwakweli wabunge wetu wote wana tutia aibu kabisa wamekuwa kama watoto wadogo.


Pengine ni kwa sababu Mwenyekiti wa muda amekuwa mpole sana na anatumia busara sana na kwakweli wabunge wanamchosha sana na bila buasra anazo tumia Mwenye kiti wa muda wa bunge maalum basi hali ingekuwa mbaya zaidi ya hii ninayo iona.

Hakika kama bunge hili maalum litaendelea kwa namna hii lazima tukubali kuwa muda ulio tengwa hauto tosha kabisa.
Wabunge wetu wameshindwa kabisa kumheshimu Mwenye kiti wa muda ndio maana wengine wanagoma kukaa hata wanapo ambiwa kukaa chini katika hili nimesikitishwa sana kuna mbunge aliambiwa akae chini aka kataa na kuanza kupiga kelele kama mtoto,Mwenye kiti alitumia busara sana kumpuuza,

Ni vyema Wajumbe wote wa bunge maalum wakajua kabisa tumewatuma wakajadiliane hili kutupatia katiba mpya nasi kwenda kupiga kelele na kuzunguka ndani ya bunge na wengine wakitoka nje na kuingia hadi ni vigumu kujua kama mjadala unaendelea maana kila mtu anafanya lake.
 
Wanajali nini, waruke sarakasi, wasinzie...washangilie kama wapo mpirani au bar.....muhimu ni laki tatu kibindoni.

Na msidhani kila aliye busy na phone pale mjengoni ana chat....face book, twitter, instagram...la hasha wengine wanatumia upande wa calculator.......busy calculating.
 
Jaribu kucheki na bunge la india. Yaani ni Noma. Nimewahi kuwa mgeni bunge la ufilipino bado tuna nafuu kubwa (simaanishi kuwa naunga mkono yanayotokea). Mungu atuepushe na majanga
 
Zile ni mbwembwe za kuingizia kipato,yaani ni furaha kwao wanapiga mayowe tu wanaingiza laki tatu.
 
Kwakweli hili bunge ni aibu tupi! Si amini kama ndio wawakilishi wetu haw! Hili ni bunge la posho sio kutunga katiba.
 
Sisi wananchi tumeanza kupoteza imani na. Bunge maalum la katiba kutokana na tabia na mwenendo wa ovyo wa wabunge
 
Back
Top Bottom