Wabunge na hadaa kwa Watanganyika kwa Cement na Bati huku wanapitisha kila kitu pale Dodoma

Wabunge na hadaa kwa Watanganyika kwa Cement na Bati huku wanapitisha kila kitu pale Dodoma

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
4,548
Reaction score
11,901
Ni bahati mbaya sana Tanzania ujinga ni mkubwa sana, Wabunge hawapimwi kwa michango yao kwa Taifa bali kwa uwezo wa kununua Cement, Bati na Misumari na kwenda kugawa Jimboni siku za weekend.

Pale Dodoma wanapitisha kila kitu kinacho jadiliwa pale na wengine hawaongei kabisa ila wanajua Jimboni wataenda na Bati za kuhadaaa wajinga.

Karinne hii bado raia wana danganywa na vitu kama misumari, bati na Cement, na wala sio kukomaa na Sera nzuri.

Kule Morogoro mbunge Abood anaweza asiongee Bungeni Mwaka mzima ila anacho fanya ni kutafuta pesa za mafuta ya Magari yake kupeleka Wafiwa misibani na kubeba maiti basi hio ndio kazi kubwa, yaani Mbunge anachaguliwa tena kwa sababu ana sapoti misiba kwa kutoa gari zibebe maiti.

Abood hawezi ongea kuhusu Tatizo la ajira, au sera za Biashara anajua wakasi wa Morogoro na wale waruguru ni vilaza tupu na wanacho penda ni kusaidiwa kubeba maiti basi.

Pale Dodoma hakuna kitu kina kwama wanapitisha theni siku za weekend kama leo wanakimbilia Majimboni mwao na mifuko ya cement kwenda kuhadaa wajinga na kuzuga na mikutano ya hadhara ya kuwahadaaa tupu.

Ni bahati mbaya nchi ina kiwango cha juu kabisa cha raia wasio jitambua huenda Dunia nzima.
 
Back
Top Bottom