Leonard Waziri
Member
- Aug 15, 2013
- 55
- 23
Na Comrade Leonard Waziri
Assalam Alaikum Mabibi kwa Mabwana Katika harakati za kuijenga Tanzania yenye Uchu wa Kupiga hatua kubwa za kiuchumi na kisiasa.
Naomba nitangulize maneno ya Waswahili, "KUISHI KWINGI KUONA MENGI"
Kupitia Msemo huu na mingine mingi ya aina kama hiyo imekua ikitumika sana kuwapa heko na pongezi nyingi wale wote waliotangulia kuliona jua na n.k.
Kupitia andiko hili sitaki kuwabeza waliotangulia hapana lakini nataka niwaombe tuangalie siasa ya sasa inahitaji nini katika maeneo yetu, sio kwamba hamjafanya lolote hapana mmefanya mengi makubwa na yenye manufaa na yanayopaswa kuigwa na hii damu changa inayokuja inakukua kwa uzalendo mkubwa katika nchi yetu,
Nawaomba sana Ifike hatua muangalie hatima yenu katika hii siasa tufike hatua tusing'atuke kwa fedheha au kufedheheshwa na vijana wadogo ambao kiumri inawezekana ni wadogo zenu au watoto wenu kabisa kisa vita ya kisiasa au madaraka mpaka ikafikia kujenga chuki na uhasama mkubwa baina yako kitu ambacho kimsingi hakina tija katika ulimwengu huu mpya wa siasa yenye kuleta Maendeleo katika Jamii zetu.
Tujenge Desturi aliyoiasisi baba wa Taifa letu Mwl. Nyerere "KUNG'ATUKA" ifike muda turuhusu damu changa yenye maono ya kuleta mabadiliko sahihi katika jamii zetu tuzipe nafasi kwa kuzielekeza na kuzishauri namna bora ya kupita katika misingi mliyoipitia nyinyi huku ikichagizwa na uchanga wake mambo yanakua mazuri zaidi, kuliko kung'ang'ania madaraka wakati muda umekutupa mkono hivyo kuyapata maendeleo kwa kasi hii iliyopo kwa sasa unakuwa mgumu sana "TUKUBALI KUNG'ATUKA"
Mathalani Kiongozi wa Nafasi ya Ubunge au Udiwani anaongoza Eneo kwa awamu 3,4,5,6 hadi 8 ambayo hiyo ni sawa na miaka 15, 20, 25, 30 hadi 40, tuulizane tu
Umeongoza miaka 10 hukufikia malengo umeongeza 15, bado tu hujafikia malengo ukaongeza miaka 20 bado tu hujatosheka?
Kwa misingi hiyo lazima kiongozi wa aina hiyo lazima ajitathmini kwa kile alichokifanya, namna jamii yake inavyomtathmini katika kuyafikia malengo ya jamii yake, kama jamii unayoiongiza imeridhishwa na namna unavyowatumikia na wanahitaji uendelee kuwatumikia kwa tathmini hiyo bado inakupa mamlaka ya kuwatumikia lakini kama tathmini ya jamii yako inakupa kizunguzungu jaribu kuzingatia maneno ya Mwl. Nyerere ya "KUNG'ATUKA"
USHAURI KWA VIJANA
Vijana Mnakila sababu ya kulitumikia Taifa hili kwa nguvu zenu zote ili tulifikishe Taifa hili katika uchumi wa kujitegemea maana safari tupo nayo kwa muda mrefu sana.
"Vijana ni Nguvu kazi ya Taifa letu" tuamke na tusimame kidete kupigania maendeleo ya maeneo yetu ya nchi yetu, kufanya hivyo Taifa letu litakuwa Taifa lenye nguvu kazi kubwa na uchumi utakua kwa kasi maana vijana ndio nguvu kazi katika kila sector, Kilimo, Afya, Uchimbaji, Mifugo, utumishi, Uvuvi, usafirishaji, Siasa, Burudani na Michezo, na sector zingine nyingi.
Mwaka 1953 Mwl. Nyerere alichaguliwa kuwa Rais wa chama cha Tanganyika African Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Makerere, hapo alikuwa na Miaka 31 Tu.
Vijana tunapaswa kulitambua hili na kutokatishwa tamaa kwa namna yeyote ile hivyo tunapaswa kutamalaki kila kona ili tulijenge Taifa letu na katika maeneo yetu, Tujitokeze kwa Wingi katika Uchaguzi Mkuu 2020 kupambana kuwa wawakilishi bora wenye Dira katika Maeneo yetu,
MWISHO
Ni kipindi cha KUJITATHMINI, Maisha ni Kupokezana Vijiti tumeumbiwa toka enzi za Mzee Adam na Hawa mpaka Leo tupo sisi, hivyo ni heri Kukabidhi kijiti kwa furaha na Upendo kuliko kukabidhi kijiti kwa Chuki na Uhasama mkubwa ambao hauna tija katika jamii yako na maisha yako kwa ujumla, Mtume Muhammad (S.A.W) Amekuwa akiomba mwisho mwema ili abaki akiwa nuru kwa watu wake, Mwl. Nyerere alisema "hapa sasa natakiwa kupumzika niwaruhusu na wenzangu waongoze"
NAOMBA KUWASILISHA
#mudawakujitathmini
#hapakazitu
#TukutaneKazini
#uchaguzimkuu2020
Sent using Jamii Forums mobile app