akajasembamba
JF-Expert Member
- Dec 24, 2010
- 1,179
- 1,794
Tunaelewa na ipo katika katiba ya nchi kwamba kazi za Wabunge na Bunge ni KUTUNGA SHERIA na KUISIMAMIA SERIKALI, kifupi ni kuwakilisha wapiga kura wake bungeni, pale ambapo serikali inagawa NATIONAL CAKE/BUDGET kila mwaka basi Mbunge naye atoe hoja ya kutetea hiyo National Cake iende kwa kiasi gani jimboni kwake, na pia kazi za Mbunge ni kupitisha SHERIA, zile sheria ambazo anaziona zitaathiri wapiga kura wake basi anatakiwa atoe hoja za kupinga kupitishwa sheria hiyo, cha ajabu tunaona wabunge wanachaguliwa kwa kutozingatia mantiki na maana ya Mbunge, kigezo kikuu na cha kwanza cha Mbunge ni UWAKILISHI na UWEZO KUJENGA HOJA, kwa niaba ya Wapiga kura wake. Inasikitisha kuona Wadanganyika wamepumbazwa na kunajisi tafsiri ya Ubunge na kugeuza kwamba Mbunge ni MFADHILI WA JIMBO badala ya MWAKILISHI wa jimbo, mbunge hatazamwi tena kwa uwezo wake wa kujenga hoja na kuwakilisha wananchi wake bungeni, badala yake ni kwa kiasi gani ametoa na ana uwezo wa kutoa misaada kwa wananchi wake, hata akienda kushona mdomo wake bungeni na kusinzia bungeni miaka 20 hatujali tena! matokeo yake bungeni zinapitishwa sheria kandamizi bajeti za kifisadi etc etc. Matokeo yake mikoa fulani imeng'ang'ania kuchagua wafanyabiashara, ambao wengi wao ni wenye asili ya kiarabu na kihindi! Na la kustaajabisha kabisa watu utawasikia wakimsifu Mbunge kwa kujenga shule, visima,kutoa vyarahani nk nk wakati mbunge huyo huyo ameachia mabilioni ya fedha yanapitishwa bungeni kama bajeti ya vitafunwa na mambo mengine ya ajabu, HATUCHAGUI MBUNGE ATOE HELA MFUKONI MWAKE, ila tunataka aibane serikali irudishe majimboni kwetu hela yetu tunayokatwa kodi kila kukicha. Mbunge akichimba kisima au kujenga shule DED,DC,Waziri nao wafanye nini na wapo kwa madhumuni gani? Au la mfumo ubadilishwe tuwe tunachagua MAGAVANA ambao watakuwa na mamlaka ya kiutawala, siyo upotoshaji ulio sasa ambao utaendeleza ufisadi. Ni muhimu sana pia Wabunge wazuiwe kuwa Mawaziri, utawakilisha vipi jimbo nawe ukiwa waziri, pia unakuwa na unfair advantage katika uwanja wa kugombea ubunge, huenda ukachaguliwa kwa uwaziri wako, hatushangai wengi waliopita bila kupingwa ni Mawaziri watarajiwa.Suluhisho wabunge na wawania ubunge wazuiwe kutoa misaada misaada ya aina yeyote ile, kwa kuwa wapiga kura wanapumbazwa na tunapata wawakilishi wabovu. Kwa kuzuiwa kutoa misaada na zawadi ndiyo wadanganyika wataelewa maana halisi ya Mbunge.