Wabunge onesheni umoja wenu kwenye suala la Katiba mpya

Wabunge onesheni umoja wenu kwenye suala la Katiba mpya

marveljt

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2017
Posts
1,503
Reaction score
1,479
Wiki iliyopita wabunge wote pamoja na mawaziri mliungana pamoja ili makonda na mwenzake waje bungeni. Wengi tulifurahishwa kwa hatua ya mshikamano huo.
Kama kweli mnania njema na taifa na siyo kwa maslahi yenu wenyewe na familia,ndugu na marafiki ,onyesheni umoja huo huo katika ile katiba iliyochakachuliwa na kuwekwa kapuni.

Wengine wataweza kusema siyo muda wake au haiko kwenye ratiba. Kuna mambo mengi yamefanyika/yanafanyika na hayakuwepo kwenye ratiba na yamefanyika. Ifike wakati tuangalie tuendako. Haya matamko na maamuzi yanayotolewa yaweze kudhibitiwa kwa mujibu wa hiyo katiba mpya. Leo hii jeuri inapatikana kutokana na hii katiba sababu anajua inamlinda.
 
Back
Top Bottom