Wabunge wa Kenya wamelaani vikali njama za utawala wa Kizayuni wa Israel za kutaka kuvuruga utulivu wa kisiasa wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Ripoti iliyotolewa inaonyesha kuwa, Wabunge wa Kenya wanaamini kwamba, utawala wa Kizayuni wa Israel umewatuma mamluki wake katika nchi hiyo kwa lengo la kuwauwa shakhsia waandamizi wa kisiasa katika nchi hiyo. Odhiambo Millie Mbunge wa kuteuliwa wa Kenya na mmoja wa waungaji mkono wakubwa wa serikali ya Rais Kibaki amesema kuwa, kuna nyaraka zinazoonyesha kuwa, mamluki hao walikuwa na mipango ya kuwauwa viongozi na shakhsia wakubwa wa kisiasa nchini Kenya akiwemo Waziri Mkuu Raila Odinga na Spika wa Bunge Kenneth Marende. Akizungumza na waandishi wa habari, Raila Odinga amethibitisha taarifa hizo na kubainisha kwamba, ana mpango wa kukutana na kufanya mazungumzo na balozi wa Israel mjini Nairobi kuhusiana na kadhia hii.
Israel haijawatuma hao mamluki ila wameitwa na wafuasi wa Rais Kibaki inavosemekana. Utawala wa Kizayuni una maana gani. Uzayuni ni manake utawala mtakatifu. Serikali ya Israel ni serikali tu kama zingine za kidemokrasi. Tofauti yao tu ni kuwa ni watu makini na wanaoishi kwa vita tokea pale waliposhindwa kutekeleza agizo la Mungu lililowataka kuhakikisha wanawaondoa wapagani waliokuwa wanawazunguka pasipo kushirikiana nao. Ukitaka mbinu za hali ya juu ya mauaji nafikiri pia ni wataalamu ila hilo haliwezi kusemwa kuwa serkali ilibariki kilichokusudiwa Kenya. Mbinu kama hizo za kukodi watu kutoka nje kumdhuru Odinga si mara ya kwanza ila mara zote watu wake wanazing'amua mapema.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.