Israel haijawatuma hao mamluki ila wameitwa na wafuasi wa Rais Kibaki inavosemekana. Utawala wa Kizayuni una maana gani. Uzayuni ni manake utawala mtakatifu. Serikali ya Israel ni serikali tu kama zingine za kidemokrasi. Tofauti yao tu ni kuwa ni watu makini na wanaoishi kwa vita tokea pale waliposhindwa kutekeleza agizo la Mungu lililowataka kuhakikisha wanawaondoa wapagani waliokuwa wanawazunguka pasipo kushirikiana nao. Ukitaka mbinu za hali ya juu ya mauaji nafikiri pia ni wataalamu ila hilo haliwezi kusemwa kuwa serkali ilibariki kilichokusudiwa Kenya. Mbinu kama hizo za kukodi watu kutoka nje kumdhuru Odinga si mara ya kwanza ila mara zote watu wake wanazing'amua mapema.