mkwapuaji
Member
- Jan 6, 2012
- 49
- 20
WABUNGE WA TANZANIA WANAWAJIBIKA KWA NANI?
Juzi kulikuwa ni kikao cha bunge kilichobeba azimio la kumpongeza Rais Samia. Sina shaka na pongezi za rais lakini shaka ni aina ya ajenda na walioamua kuibeba ajenda.
Matatizo ya kujadili kama WABUNGE wanaowakilisha wananchi zaidi ya milioni 60 ni mengi na sikuona sababu ya kuacha kujadili namna bora ya kumsaidia mwananchi huyu tuanze kujadili namna ya kumpongeza kiongozi kwa kutimiza majukumu yake.
Labda niseme, majukumu ya raisi ni halali kwa yeye kuyatimiza na wala hapaswi kukumbushwa wala kuombwa kwakuwa ameapa kuyatekeleza na ana wajibu wa kuyatekeleza. Kama ilivyo kwa majukumu ya bunge kwa raisi na serikali pia katika kuwajibishana.
Kilichofanyika hapa ni kupeleka ujumbe wanaoutaka wao hasa kutaka wafikiriwe kisiasa na raisi kwa kivuli cha pongezi angali kama WABUNGE wana majukumu ya kuisimamia na kuiwajibisha serikali.
Tumeona mengi tu toka kwenye ripoti ya CAG yaliyopaswa kujadiliwa. Tumeona mengi hasa utendaji wa baadhi ya mawaziri ambao wanafuja mamlaka yao na WABUNGE wapo kimya tu.
Tumeona namna teuzi zinavyofanyika kwa kujirudia kwa sura zilezile huku malalamiko yakizidi kuongezeka na WABUNGE wameweka nta masikioni na midomoni hawataki kabisa kujadili kwanini waliokosea wanaendelea kuzungushwa kwenye nafasi angali wapo watu wengi tu wanaoweza kusaidia
Tumeona taasisi nyingi za serikali zikilia hasara angali tunaona taasisi zifananazo kimaudhui nazo za binafsi zikikua kwa faida ni lini bunge limejizatiti kuyajadili haya? Wapi wamehoji kufanikiwa kwa Fastejet, Vodacom, kampuni za mabasi na kufeli kwa Air Tanzania, TTCL na TRC. Aina ya watu wanaoteuliwa kuyaendesha haya ni ileile ya waliofeli na wasio na weledi lakini WABUNGE wanaazimia kusifia wajibu.
Yaani ni sawa na waumini kumsifia Sheikh ama Padre kwa kufanya ibada sasa walitaka afanye nani?