Wabunge wa CCM kumpigia debe January Makamba kwa namna alivyofeli ni kuwakebehi na kuwadharau Watanzania

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Hivi kweli huyu Makamba ni wa kumpigia debe kwa kejeli namna hii? Eti inafikia hatua baadhi yenu mnadai sasa Msambaa kapewa zigo na amelifikisha hii ni kebehi kubwa.

Mpaka sasa nishati ya umeme ni tatizo hapa nchini. Maana kila siku ni umeme kukatika hovyo.

Tangu awe waziri ni harufu ya ufisadi na ujanja tu ndani ya hii wizara ya nishati. Ukarabati wa miundo mbinu usiokwisha na kandarasi za kijanja kijanja kama ya Mahindra Tech. Lakini hakuna tija kwa wananchi.

Inashangaza sana kuona wabunge mnasifia upuuzi huku wananchi wakiumia kwa kukosa nishati ya uhakika huku bwawa la JNHP likidorola kwa sababu za ajabu ambazo ni upigaji pesa wa kiroho usio na huruma kwa raia.
 
Hivi kweli huyu Makamba ni wa kumpigia debe kwa kejeli namna hii? Eti inafikia hatua baadhi yenu mnadai sasa Msambaa kapewa zigo na amelifikisha hii ni kebehi kubwa...
Yataisha tu na tutamsahau huyo Febuari
 
Huku kwetu umeme tunausikia tu ,kata yote hatuna umeme sijui tumeikosea nini serekali ,Mama umefanya mengi sana mazuri tunakuomba kata ya lugulu ilipo same tupatiwe umeme
 
Waliompamba walipewa mlungula,kupata control number ya malipo Tanesco ni karne inapita. ukishalipia, kuunganishiwa subiri jirani na uchaguzi. Umeme ukiingia tu TOOZO hadi kupukuta vumbi kwenye nyaya.

Ni bora mtu akipata kuwa tu ajaze fomu ya Tanesco
 
Hivi kweli huyu Makamba ni wa kumpigia debe kwa kejeli namna hii? Eti inafikia hatua baadhi yenu mnadai sasa Msambaa kapewa zigo na amelifikisha hii ni kebehi kubwa...

CCM wamejenga utaratibu mbaya wa kusifia chochote kinachofanywa na kiongozi wao, na muasisi wa tabia hii ni dhalimu. Sasa sijui unashangaa nini wakati ni tabia mliyoilea wenyewe.
 
CCM wamejenga utaratibu mbaya wa kusifia chochote kinachofanywa na kiongozi wao, na muasisi wa tabia hii ni dhalimu. Sasa sijui unashangaa nini wakati ni tabia mliyoilea wenyewe.
Ukiona hivyo ujue wamepokea rushwa safi
 
Waliompamba walipewa mlungula,kupata control number ya malipo Tanesco ni karne inapita.ukishalipia,kuunganishiwa subiri jirani na uchaguzi.Umeme ukiingia tu TOOZO hadi kupukuta vumbi kwenye nyaya.
Ni bora mtu akipata kuwa tu ajaze fomu ya Tanesco
Tupe ushahidi wa mlungula waliopewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…