Wabunge katika nchi zote wanatakiwa kuwa mfano kwa jamii wanayoingoza na hasa kwa vijana. Jamii inategema kuwa sheria na kanuni zinazotungwa na wabunge kwanza kabisa zinatakiwa ziheshimiwe na kufuatwa na wabunge wenyewe.Sheria ya kuongoza Benki kuu ya Tanzania katika shuhuri zake ililtungwa na bunge na ili kufanikisha kazi zake Benki kuu nayo ina kanuni zake ambazo wabunge wanatakiwa waziheshimu; moja ya kanuni hizo ni kuwa ili kuondoa mgongano wa maslahi, wabunge hawatakiwi wawe wakurugenzi wa bodi za benki za umma, hata hivyo wabunge wa ccm wamekaidi agizo hilo toka benki kuu na kuendelea kuwa wakurugenzi wa benki hizo. Je kwa kukaidi agizo la benki kuu Waziri mkuu hapaswi kuhakikisha kuwa wabunge hawa wanaondolewa badala ya kuwa mfano mbaya wa kukosa maadili kwa vijana wetu?