ELNIN0
JF-Expert Member
- Nov 26, 2009
- 4,161
- 1,476
Ningependa kuwauliza wabunge wa CCM na wana JF kwa ujumla mtazamo wao kama kweli wapo nyumba na spika wao Samweli Sita katika kutekeleza maamuzi mazito ya nchi au kutetea maslahi ya taifa hili kwa ujumla. kwa mafano kama Sita angenyanganywa uananchama kwenye CCM je nyie wabunge mngekufa pamoja na spika wenu? au yangekuwa yale yale ya kutosana. (Kheri mimi sijasema..)
Tatizo linakuja pale ambapo serikali itashindwa kutekeleza mapendekezo ya kamati za bunge, je wabunge mtakuwa sambamba na spika wenu kufa kifo kimoja kwa maslahi ya taifa letu?
Kwa mtazamo wangu Samweli anakuwa Spika wa kwanza kufanya kazi yake vyema, binafsi nampongeza sana, si kazi rahisi ukizingatia anatoka humo humo ndani ya chungu cha CCM, naunga mkono kwamba ukitaka kummaliza adui yako mmalize humo humo ukitoka nje hutamweza.
Unaongoza bunge kwa usawa, hoja ndizo zimetawala na hili ni zuri mno kwa sisi wananchi wa hali ya chini, tunapata watetezi.
Watu walifuatilia sana mambo yako hadi ulipokwenda Urambo iliuwa talk of the town, wakuu wako wa chama wakashituka wakakufuata huko huko kuomba msamaha na kuweka mambo sawa, wewe muungwana na IQ ipo juu.
Samweli usije kuwa Mbuzi wa kafara kaka yangu, haya mambo yaangalie kwa makini, nachoomba mungu akujaze roho ya ujasiri, akulinde na ututumikie sisi watanzania wanyonge.
Sipati picha kama wewe Samweli ungekuwa pamoja na hawa mafisadi, kweli tungekuwa pabaya sana, leo hii tunaongea Richmood, Buzwagi, Kiwila na mengineyo bila kuogopa. Pia kwa mara ya kwanza serikali inajiuzuru mikononi mwako, spika mwoga angesema anaumwa anaenda kutibiwa nje ya nchi lakini ukasema nitalikabili hilo, si jambo rahisi.
Mengine machache yapo kama EPA mfano kagoda , Mwananchi gold na meremeta bado yana kizuizi sasa sijui kwa maslahi ya nani maanayake taifa si ni sisi wenyewe na nyie ndiyo mnatuwakilisha.
Nakupa hongera sana ila naomba wabunge wenzako wawe pamoja na wewe na mungu akubariki sana spika wangu - ukirudi 2010 tumalizie kazi iliyobaki ili uingie kwenye vitabu vya kumbumbu ya taifa letu.
Mwsho wakikukaba sana humo, basi hata sisi tunakuhitaji uje tuongeze mashambulizi
Asante.