johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Wabunge wastaafu na wale watarajiwa wa CCM wamejianzishia mtaa wao huko Ununio na kuuita Bunge Btreet, miongoni mwao ni Mzee Kimiti, Mh. Foya wa Hai, Mh. Adam wa Muleba na Mh. Kippi anayetarajia kugombea Kawe.
Cha kusikitisha wabunge hawa wamefunga barabara na kuzuia mkondo wa maji hali iliyopelekea eneo lote la mtaa wa Mombo kujaa maji kwa takribani miezi mitatu sasa.Wananchi wa eneo hilo wamemwendea diwani wa Kunduchi Mh. Urio ili awasaidie lakini awali Urio alidai hao wabunge ni mabosi wake ila atatafuta namna " nzuri" ya kuongea nao.
Baada ya kuongea nao serikali ya mtaa iliagiza wananchi wachangie sh 50,000 kila nyumba ili ujengwe mtaro lakini baada ya fedha kuchangwa diwani hapatikani wala hapokei simu.
Wananchi hao wamedai kuwa mambo ya UONEZI, dhuluma na unyanyasaji kama hayo ndio huwatia hasira na kuamua kuwachagua wapinzani.
Hadi sasa inaelezwa mafuriko hayo yamesababisha kifo cha mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Makaranga aliyefia ndani ya nyumba kwa kukosa msaada.
NB: Mh. Diwani Urio najua unapita humu nenda katatue kero za wapiga kura wako
CC: RC Makonda
CC: H. Mdee (MB)
Maendeleo hayana vyama