Wakuu,
Mtiririko hua uko hivi:
Mhe. Spika anasema anayefuatia kuchangia ni Mheshimiwa kipele uchungu, mheshimiwa mbunge kipele uchungu anaanza:
1. Kwanza Namshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma
2. Pili nakushukuru wewe mheshimiwa spika kwa jinsi unavoongoza vizuri bunge letu
3. Tatu namshukuru muheshimiwa Rais kwa anavojituma sana kuwasaidia Watanzania bila kubagua.
4. Nne napenda nimshukuru mke wangu maana bila yeye hata hivi kazi mimi nisingeziweza
5. Tano nawashukuru wapiga kura wangu jimboni na najua muda huu wananiangalia kwenye TV wajue kabisa mbunge wao nawapambania.
Mkumbuke amepewa dakika tano dakika tatu kazipiga kwenye shukrani mbalimbali, sasa dakika mbili zilizobaki ndio anaeleza kero kama ifuatavo:
Mheshimiwa spika, kuna matatizo makubwa ya maji katika kijiji cha Lupongo, pale mkandarasi ana miaka mitano hakuna kitu.
Mheshimiwa spika, kuna ile barabara ya Kijichoupande kwenda hadi Malowe haipitiki yaani wananchi wanateseka sana kama waziri anaweza twende nae akajionee mwenyewe.
Halafu vituo vimejengwa vya afya lakini hakuna manesi wala madaktari na vifaa tiba hakuna
Mheshimiwa spika wananchi wamevuna ufuta lakini soko hakuna hii inanisikitisha sana sijui hata itakuaje msimu ujao.
Mara kengele kreeee kreeeee!
Mbunge anauliza hii ya kwanza au ya pili? Spika anamjibu ya pili hiyo.
Sawa mheshimiwa NAUNGA MKONO HOJA LAKINI NILIYOSEMA MZINGATIE hapo wa jirani yake wanagonga meza kumpongeza kuashiria kua amefanya kazi kubwa halafu anafunga mike anakaa kwa raha zake mambo yanaoshia hapo.
Nadhani mnaona sio tena kuisimamia serikali na kuishauri bali wanageuka watu wa kuisifu serikali kwa wabunge wa namna hiyo hatutoendelea kamwe kila siku mambo ni yale yale.