Na bado....
Hiki chama kama kimelaaniwa vile.
Wakome kupitisha sheria ya kuzuia mgombea binafsi...
Sasa linawarudia...
.Kuhamia Chadema siyo suluhisho, tunataka tujue ni akina nani hao, usije ukakuta ni EL, RA na Chenge! ebo
Mkuu hujui kuwa wagombanao ndio wapatanao?Kati ya Chadema na CUF, nadhani CUF ni better. CHADEMA kuna ugomvi sana. Chadema wanaweza kujirekebisha, na muda upo wa kujirekebisha,lakini sasa wana siasa za kutwangana makonde ndani ya Chama.
Mivutano ndani ya CCM imewafanya baadhi ya wabunge wa CCM kuomba ushauri toka kwa wahadhiri wa fani ya Siasa wa UDSM ili kukabiliana nazo ikiwemo uwezekano wa kuhamia CHADEMA! Wabunge hao wa CCM (majina yao hayajafahamika) wamedai kuwa kuna kampeni za chini chini majimboni mwao kwa kuwa kuna wanaogawa fedha ili kuwabwaga, hali ambayo imekuwa tete kwao! SOURCE: HabariLEO, tr 15/11/2009.
Msishangae kukuta ni wale wale ambao wananchi wanataka kuwabwaga majimboni kwao kwa kushindwa kutimiza ahadi zao.
Vilio vingi vinavyotokea sasa ni vya kutaka kuonewa huruma. Kwa mtu aliyetimiza wajibu wake, hata nani aende kumwaga mapesa, huyo mbunge atashinda tu. Lakini kwa wale ambao waliyahama majimbo yao kwa miaka minne, hata waende chama gani watadondoshwa tu.
Hakuna kitu kama hiki Mtanzania.
FairPlayer,
Mimi namjua mbunge mmoja ambaye analia lia na kila anayetaka kugombea jimbo lake anamwita fisadi, anadai kuna mapesa yanamwagwa. Sasa kama kuna mapesa yanamwaga si aende polisi? Si aende PCCB? Si awataje majina hao wanaomwaga pesa? Si awataje majina hao wanaodhaminiwa? Si awataje majina wananchi hao wanaopewa pesa?
Nitakuwa wa mwisho kuamini vilio vya wabunge kama hao kwasababu wengine hata tumehusiswa na ufisadi wakati ukweli uko tofauti kabisa.
Wacha kipenga kilie na tutawaambia mbele ya wananchi wathibitishe hizo tuhuma zao. Kuchafua watu bila sababu zozote ni ufisadi mkubwa kuliko hata huo wanaojifanya wanaupigania.
Amani inajengwa na fairness na uongozi wa haki na sheria. Haiwezekani nchi ikaruhusu watu wachache kwasababu wanadhaminiwa na wamiliki wa vyombo vya habari, wakaamua kuwachafua wapinzani wao bila kuwa na ushahidi wowote. Huo sio uongozi, ni ujambazi wa kisiasa.
Labda kumbukumbu zako ni mbovu; Sophia amewataja kwa majina anaowatuhumu.Mipasho hii.....una undugu na mh Sophia Lioness? Kwanini usimtaje huyo Mbunge kama una guts? Ifikie wakati tuende na facts....MBUNGE MMOJA....Mbunge fulani duuuuuuuuuuuu Mkuu vipi bwana!
Siasa za majimbo hazipiganiwi JF.