Bunge la kenya limekuwa kali kusimamia maslahi ya wakenya hadi katiba mpya kupatikana.Pia wamesimamia bajeti kikamilifu kiasi kuwa bajeti ya Kenya inategemea mapato yao wenyewe ya ndani bajeti yao si tegemezi kama ya kwetu.
Hivyo wanastahili pongezi kwa kujali maslahi ya wakenya na usimamizi mzuri wa mapato na matumizi na kuifanya bajeti isiwe tegemezi.
Hivyo wanahaki kulipwa.
Hawa wabunge wa Tanzania naomba si tu wafutiwe posho naomba hata mishahara yao ipunguzwe walipwe kima cha chini.
Si wabunge tu hata raia wa kenya ni tofauti na wa tanzania,nasema hivyo kwa yafuatayo 1.wamesimamia kidete kupata katiba mpya ambayo inamujali wanjiku(mwananchi wa kawaida) mfano mzuri wwa katiba yao ni kupunguza madaraka ya raisi,hebu tuangalie jinsi majaji,,mwendesha mashitaka mkuu na wengineo walivyochaguliwa baada ya kupitia vipima joto ambavyo ingekuwa ni hapa sijui ingekuwaje2.angalia wanachi walnavyoshinikiza wabunge wao walipe kodi katika posho zao,je wa kwetu si mumewasikia wanavyompinga zitto na sisi wananchi tumeusugua 3 mafuta ya petroli yalipopanda pamoja na sembe wakenya waliingia mitaani hadi serikali ikajirudi,je sisi hapa bongo tumefanya nini 4.nachelea kusema ingekuwa ndio Kenya huu mgao wa kukaangwa wa tanesco pasingetosha lakini je sisi wa TZ ndio mwanzo tunapiga miluzi na bwana mkubwa ndio anazidi kupasua anga,hajali na hakuna anayejali,watanzania tuna matatizo makubwa ya unafiki na kutojiamini
Naomba kutoa hoja