Wabunge wa Lowassa wamerudi CCM na kumpa majibu Dr Slaa kwamba mzee wao alikuwa ni Liability kwa CHADEMA!

Unajua hayo maneno "Asset" na "liability" yalikuwa na uthamani wakati gani?
Mpaka sasa bwashee....... Ni kama nyumba unayojenga kwenye kiwanja cha " kienyeji" ni tofauti na ya kiwanja chenye hati na matokeo yake huonekana baadae mji unapozidi kukua bwashee!
 
Dk. Slaa akisema neno jua litatimia.
Sasa hivi wanaona aibu hata kuvaa Tshirt na magwanda
 
Jo naona unateseka sana na CHADEMA... Ila kumbuka hili ni chama la wana.. Halifi kesho wala keshokutwa.. Litadumu miaka 1000View attachment 1463733

Jr[emoji769]
Dah kuna watu ni ngumu kuelewa akiki zenu kama zinaitakia mema Tanzania. Hata kama ni uchaga mmezidi Mshana Jr . Tunajua jinsi mlivyoiba hela kibao na kuua wanaowapinga ila tusimamie ukweli CCM ni baba yako pia.
 
CCM ilipoteza kule kuaminika kabla ya uchaguzi wa 2015, hivyo uwepo wa Lowassa kama mgombea wa upinzani ukaonekana ni wa muhimu sana.

Iwapo Magufuli angekuwa rais mwaka ule kuelekea uchaguzi mkuu na akawa ni mtendaji kama alivyo sasa huyo Lowassa asingepata hata nusu ya kura alizozipata.

Udhaifu wa CCM ile ndio ulikuwa uimara wa Lowassa yule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…