Kenyan
JF-Expert Member
- Jun 7, 2012
- 414
- 314
Polisi wamelazimika kutumia vitoa machozi kutawanya Wabunge wa Upinzani waliowasili nje ya Ofisi ya Rais wakitaka kumkabidhi Rais barua inayodaiwa kueleza kwa kina matakwa ya Muungano wa Azimio.
Wabunge wakiwemo Edwin Sifuna, Babu Owino na Otiende Amollo wamesema ni haki yao kuandamana kwa amani na haikufaa Polisi kuwarushia mabomu ya machozi.
Mpaka kufikia sasa Polisi wamefanikiwa kuzuia waandamanaji kuingia kati kati ya Jiji japokuwa hali ni tete katika Barabara ya Mombasa inayoelekea Uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta. Aidha eneo la Kibra na Mathare Hali pia sio salama.
Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga bado hajajitokeza hadharani leo.