Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
WABUNGE WANAWAKE ZANZIBAR WAFIKA KASKAZINI UNGUJA, WAKAGUA MIRADI ILIYOTEKELEZWA
Wabunge Wanawake Zanzibar wakiwemo Wabunge wa Majimbo na Wabunge wa Viti Maalum wameendelea na ziara yao ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi
Katika kukagua miradi, Wabunge Wanawake Zanzibar wameeleza kuwa jitihada za Serikali katika
Kuimarisha huduma za afya kwa kujenga Hospitali za kisasa karibu na maeneo ya wananchi kumesaidia sana kupunguza vifo vya mama na mtoto kipindi hiki ambacho kuna ongezeko la watu kila siku.
Wakiwa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja Wabunge wa Viti Maalum na Wabunge wa Majimbo Wanawake wamesema kuwa hatua ya Serikali ya kutekeleza miradi mbalimbali na mikubwa
italeta ustawi mzuri kwa Wananchi kwani wananchi siku zote wanahitaji urahisi wa kupata huduma bora na ni jukumu la Serikali kupeleka huduma kwa wananchi
Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini A, Mhe. Rashid Simai Msaraka na Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B, Mhe. Juma Sururu wamesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kuendelea kuleta maendeleo makubwa kwa wananchi wake ili kukuza Uchumi wa Nchi na kuleta huduma bora za kijamii
Aidha, Wakuu wa Wilaya wa Kaskazini A na Kaskazini B wamefahamisha kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imefanya mageuzi makubwa katika maeneo mbalimbali ya Mijini na Vijini ili kuondoshea usumbufu waliokuwa wanaupata Wananchi.
Hata hivyo, Wakuu wa Wilaya ya Kaskazini A na Kaskazini B wamesema kuwa Serikali zote mbili zimefanya kazi kubwa ya kuhakikisha maendeleo yanapatikana katika Sekta mbalimbali na wananchi wanaishi katika mazingira wezeshi na salama.
Ziara ya Wabunge Wanawake Zanzibar imefanyika kwa kutembelea miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo Kituo cha afya Nungwi, Barabara za ndani na Uwanja Ndege, Hospitali ya Wilaya Kivunge, Skuli ya Ghorofa Bumbini, Tanki la Maji Bumbwini na Mradi wa Bandari Mangapwani
Attachments
-
WhatsApp Image 2024-11-30 at 09.27.08.jpeg483.5 KB · Views: 9 -
WhatsApp Image 2024-11-30 at 07.47.47.jpeg330.6 KB · Views: 8 -
WhatsApp Image 2024-11-30 at 07.47.46.jpeg396 KB · Views: 9 -
WhatsApp Image 2024-11-30 at 07.47.53.jpeg658 KB · Views: 8 -
WhatsApp Image 2024-11-30 at 07.47.48.jpeg371.2 KB · Views: 9 -
WhatsApp Image 2024-11-30 at 09.26.12.jpeg587.6 KB · Views: 8 -
WhatsApp Image 2024-11-30 at 07.47.58.jpeg582.9 KB · Views: 8 -
WhatsApp Image 2024-11-30 at 07.47.56.jpeg457 KB · Views: 7 -
WhatsApp Image 2024-11-30 at 07.47.55.jpeg450.4 KB · Views: 7 -
WhatsApp Image 2024-11-30 at 07.47.54.jpeg140 KB · Views: 10