Wabunge washinikize taasisi za serikali na binafsi wagaramie wote wanaowaita kwa interviews

MARKYAO

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2012
Posts
673
Reaction score
681
Limekuwa ni tatizo sugu hususan kwa taasisi za serikali kuita wasaka ajira masikini kutoka maeneo mbalimbali ya nchi bila kuzingatia haki za binadamu kwa kuwalipa gharama za usafiri, malazi na nyinginezo. safari moja inagharimu mpaka Sh 200,000 kwa mtu anayetoka Kigoma au Buboba kwa basi, achilia mbali risks na changamoto nyingine za njiani. wanaitwa watu wengi kwa aptitude test na selection ya oral wachache na kwa mda wote gharama za kufanya interviews hizi zikiwz ni kubwa kwa sisi masikini na tusioishi Dar es Salaa.

Mifano ya taasisi za serikali ni nyingi sana mfano TRA, Tan Roads, PCCB, TPDC nk. Naomba nichukue mfano wa TPDC, ambapo recently waliita accountants 672 kwa aptitude test na walikuwa selected only 24 kwa oral Interview kwa nafasi 6 tu. Maendeleo ya Jamii waliitwa 368 wakatoka 16 kwa oral kwa ajili ya nafasi 4 tu. Kwa nini wanaita watu wengi namna hii na wanajua hawacompensate travel and accommodation expenses? Hawa wote wamelazimishwa kuomba Kazi kwa kutumia S.L.P. Posta wamekula 1,100 ya stamp, achilia mbali printings and photocopies, plus Pasport size photo! Huu si wizi wa taasisi hizi na kuzidisha umaskini kwa vijana wanaohangaika miaka na miaka kutafuta kazi?

Naomba Wabunge watafiti hili suala na pia watueleze umuhimu wa Secretariat ya ajira kwani ndo wameongeza hujuma kwa Vijana wanaotafuta ajira. Serikali iwajibike kwa kuwa hawa vijana wamesoma vyuo ambavyo wamevifanyia accreditation na kuona vinafaa na wahitimu wake wapewe ajira. wizara ya kazi itengeneze opportunities kwa vijana transparently sio kusema kwenye majukwaa ya siasa huku wasinzia kusaidia vijana kupata ajira za kueleweka.
Wizara wapige marufuku course ambazo wanaona hazina tija kwa taifa na wanafunzi na sio kufurahia utitiri wa vyuo feki huku vijana wakishindwa kupata mwongozo utakaowasaidia katika maisha zaidi ya siasa.

Wanau Nawasilisha na kama kuna watakaoguswa kwa njia moja au nyingine waendeleze kwa michango constructive ili walengwa wapate ujumbe na kuwajibika ili kutunusuru vijana.
 
Ni kweli ,harafu sometime mnabebeshwa mzigo wa gharama wakati kazi yenyewe washajulikana wakupewa..watu hawana huruma aiseee. Wao ndio wawe wanagharamia kila kitu katika interview kwani wao angalau wana uhakika watapata mfanyakazi wamtakaye,kulipo watu 600 kugombania nafasi 4, gharama zote wakati probability ya kupata kazi ni 4/600.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…