Abdulhalim
Platinum Member
- Jul 20, 2007
- 17,215
- 3,076
Hii ndio ukisikia typical example ya serikali suruali. no vision no nothing! fuatilia hii habari kutoka mwananchi.
Wabunge washtushwa ATCL kudaiwa 39 bilioni
Sadick Mtulya
Gazeti la Mwananchi
WAJUMBE wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, wameshutshwa na deni la Sh39 bilioni na gharama ambazo Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), zinalilipa Shirika la Ndege la Air Bus.
Deni na gharama hizo zinatokana na ndege ATCL iliyopata hitilafu ya bawa, wakati ikitua mkoani Mwanza siku kadhaa zilizopita.
Kutokana na hali hiyo, kamati hiyo imeitaka Bodi ya ATCL inayongozwa na Balozi Mustafa Nyang'anyi, kuwasilisha vilelezo vya mikataba kati ya Shirika la Ndege la Air Bus na ATCL.
Mikataba hiyo inapaswa kuwasilishwa bungeni katika kikao kinachotarajiwa kuanza wiki ijayo.
''Ni kweli ATCL inadaiwa Sh39 bilioni na kulipa gharama za ile ndege iliyopata hitilafu kule Mwanza. Fedha hizo zinalipwa Shirika la Ndege la Air Bus. Kutokana na hilo kamati imeiagiza bodi ya ATCL kuleta vielelezo vya mikataba iliyongia na shirika hilo katika Bunge la linaloanza Aprili mwaka huu,'' alisema Mwenyekiti wa kamati hiyo Mohamedi Misanga.
Misanga alisema kamati yake itatangaza msimamo wake baada kupitia vielelezo hivyo na kupata maelezo ya kina.
Mapema, kamati hiyo ilikutana kwanza na wawikilishi wa wafanyakazi na kupokea mapendekezo yao.
Baadaye ilikutana na bodi kwa ajili ya ufafanuzi wa mambo mbalimbali ya msingi.
Baadhi ya wabunge waliozungumza na gazeti hili, wameapa kuibana ATCL ili itoe taarifa za msingi kuhusu matatizo ya kimejimenti, tangu shirika hilo liliporejeshwe mikononi mwa wazalendo, baada ya kuvunjwa mkataba kati yake na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA).
"Tuliwabana hadi wamevunja mkataba na SAA, tumewapa wazalendo wenzetu mambo bado hayaendi kabisa, mara unasikia ndege iliyonunuliwa bawa moja lina itilafu," alisema mbunge mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwa.
1. Wamestushwa? Really? Wabunge wamestushwa kana kwamba kadhia kama hii ni mpya(?)..
2. Wabunge wanaomba mkataba baina ya ATCL na Airbus? Wabunge sasa wamekuwa Ernst and Young au wamekuwa wajuvi wa kila kitu a.k.a wazee wa theory of everything. Technically, ni vema ikumbukwe wabunge sio part ya utekelezaji ktk serikali, na mfumo uliopo they can go to hell and whatever they think kwa sababu serikali inayohaki ya kukataa kushare opinion zao, hata iweje isn't it?Sarakasi!