Wabunge wameitaka Serikali kukokotoa upya bei ya umeme baada ya mradi wa kufua nishati hiyo wa Julius Nyerere (JNHPP) kukamilika ili kumpa nafuu Mtanzania.
Akiuliza swali la nyongeza bungeni leo Agosti 30, 2024, Mbunge wa Lupa, Masache Kasaka amesema mradi wa JNHPP umeanza uzalishaji umeme wa kutosha na kuna wa ziada.
Kutokana na hilo amehoji, “je, Serikali haioni haja ya kupitie upya ukokotoaji wa bei za uniti na baadaye kushusha bei ili kuleta nafuu kwa Mtanzania?”
Soma Pia: Nashauri Serikali kupunguza bei ya umeme kuchochea shughuli za kiuchumi
Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga katika majibu ya swali hilo amesema gharama za umeme si za uzalishaji peke yake, bali zinahusisha za usambazaji, usafirishaji na uwekezaji.
Hata hivyo, amesema kwa kuangalia bei za nishati hiyo katika nchi nyingine za Afrika Mashariki, Tanzania ina bei ya chini.