Wabunge wameitaka Serikali kukokotoa upya bei ya umeme baada ya mradi wa kufua nishati hiyo wa Julius Nyerere (JNHPP) kukamilika ili kumpa nafuu Mtanzania.
Akiuliza swali la nyongeza bungeni leo Agosti 30, 2024, Mbunge wa Lupa, Masache Kasaka amesema mradi wa JNHPP umeanza uzalishaji umeme wa kutosha na kuna wa ziada.
Kutokana na hilo amehoji, βje, Serikali haioni haja ya kupitie upya ukokotoaji wa bei za uniti na baadaye kushusha bei ili kuleta nafuu kwa Mtanzania?β
Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga katika majibu ya swali hilo amesema gharama za umeme si za uzalishaji peke yake, bali zinahusisha za usambazaji, usafirishaji na uwekezaji.
Hata hivyo, amesema kwa kuangalia bei za nishati hiyo katika nchi nyingine za Afrika Mashariki, Tanzania ina bei ya chini.
Mitambo kwani inaendeshwa na nani?.
Wapo waandisi wanaolipwa kwa kazi hiyo pamoja na ukarabati na matengenezo,bei zishuke raia wahamasishwe kupika kwa kutumia umeme kuokoa mazingira
Wabunge wameitaka Serikali kukokotoa upya bei ya umeme baada ya mradi wa kufua nishati hiyo wa Julius Nyerere (JNHPP) kukamilika ili kumpa nafuu Mtanzania.
Akiuliza swali la nyongeza bungeni leo Agosti 30, 2024, Mbunge wa Lupa, Masache Kasaka amesema mradi wa JNHPP umeanza uzalishaji umeme wa kutosha na kuna wa ziada.
Kutokana na hilo amehoji, βje, Serikali haioni haja ya kupitie upya ukokotoaji wa bei za uniti na baadaye kushusha bei ili kuleta nafuu kwa Mtanzania?β
Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga katika majibu ya swali hilo amesema gharama za umeme si za uzalishaji peke yake, bali zinahusisha za usambazaji, usafirishaji na uwekezaji.
Hata hivyo, amesema kwa kuangalia bei za nishati hiyo katika nchi nyingine za Afrika Mashariki, Tanzania ina bei ya chini.
Mimi nashauri serikali ipandishe bei ya umeme iwe mara tatu ya bei ya sasa.
Na ikiwapendeza, serikali iongeze kodi ya electricity levy kwa kiwango cha 20%.
Watanzania wana hela, we angalia magari yaliyo barabarani yalivyo mengi na yote ni namba E tu.
Ambaye ataona bei ya umeme ni kubwa ahamie Burundi