Wabunge wengi wamelala usingizi wa pono. Hawasemei miradi iliyotekelezwa maeneo yao

Kwa hiyo ulitaka vijengwe wapi?
 
Mbona uwanja wa mwamza hauitwi uwanja ilemela bali unitwa mwanza huku kuna mtu wa magu pengine hajawahi kuuona lakini nae ni sehemu ya mwanza?
Sasa hivi hadi wanajistukia kutamka Uwanja wa ndege wa Chato mara kadhaa wanauita Geita.
 
[emoji2][emoji2][emoji2] Yaani wabongo mna nongwa, kwani uwanja mkubwa ukijengwa Chato Kuna shida gani? Taifa stars ikichezea Chato Kuna shida gani? Kwani Mikoa mingine hakujengwi viwanja? Chato siyo Tanzania?

Kahama iko mkoa wa Shinyanga ambako Aiport ya Shinyanga inapanuliwa na itakuwa na uwezo wa kupokea ndege kubwa Kama dreamliner. Chato iko mkoa wa Geita, kwa hiyo Aiport ya Chato ni ya mkoa wa Geita.

Kuhusu Hospitali za Kanda nimefafanua vya kutosha wanapoweka location ya Hospitali lazima wafanye tathimin namna gani itanufaisha pande zote. Pia Cha kuongezea location ile itavutia hata medical tourism kwa nchi jirani Kama Uganda na Kenya.
 
Uwanja unaojengwa Chato ni wa pili kwa ukubwa baada ya ule wa Mkapa!Umewaza ingekuwaje kama Mkapa angeenda kujenga huo uwanja alikozaliwa?
Wilaya gani nyingine nchini ina neema ya kupata uwanja wa kimataifa wa mpira wa miguu kama Chato?
Kuhusu hospitali ya rufaa,nimesema hata kijiografia hospitali haikupaswa kuwa Chato kama lengo ni kuhudumia Kigoma,Rukwa,Kagera na Shinyanga!Walau ingejengwa nyakanazi!Mtu kutoka kigoma itabidi apige KM zaidi ya 600 kwa barabara kufika Chato,huo ni uungwana?Vp mtu kutoka Rukwa?Acheni siasa za rejareja!
Eti utalii wa hospitali,mtu atoke Nairobi au Kampala ambako kuna hospitali kubwa na za kisasa aje kushangaa hospitali Chato?Are you serious?Kabisaa?
Kama ni Airport basi ilipaswa kuwa makao makuu ya Mkoa yaani Geita na si huko Chato!Mtu ni bora akashukia Mwanza na kuja Geita kwani ni karibu kuliko kushukia Chato halafu aitafute Geita ambako kunakuwa mbali zaidi!

Punguzeni mahaba na muwe wakweli kwa nafsi zenu!
 
Again why chato na sio muleba au kasulu?

Ishu hpo ni coincidence ya magufuliMagufuliMagufuliMagufuli
Hii inaonyesha kbsa kuna kitu hakipo Sawa ila kwa kuwa watanzania unafiki ishakuwa ni sehemu ya maisha yetu ndyo maana tunaona hii ni Hali ya kawaida.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Kwanini atangulize kwake, alafu kwingine kutajengwa?
Hapo ndipo tunaona kunipendelea.
Zamani wazazi hasa wakiume, unatengwa wali kwa nyama, mtoto hakuruhusiwa Kula nyama mpk aruhusiwe na baba.

Huyo baba atashambulia nyama baadae atasema kuleni na nyama! Wababa wengine waligawa vibande kwa Kila mtoto, vitakavyobaki vinamuhusu yeye. JE HAUKUWA UROHO NA ULAFI?

NDIVYO ALIVYO HUYU KWENYE KEKI YA TAIFA.

Angekuwa mcha Mungu angetanguliza mikoa wilaya zingine.
Ndivyo neno la mungu linavyoagiza.
 
Acha kukwepa,hebu jibu moja kwa moja.
Unaifahamu Geita?Kwa uelewa wako unadhani mkoa wa Geita ni wa kubebwa na mji mdogo wa Chato kimapato?Tembelea mkoa wa Geita uuone, Don't be an armchair thinker!
 
Huwa Kuna msemo fulani hivi, kwamba ukileta machungwa nyumbani,halafu unaishi na watoto ambao sio wa kuzaa wewe;Basi anza kuwapa watoto wasio wa kuzaa wewe,ili wawakatie vipande watoto wako wa kuzaa.Msemo huu una maana kubwa sana.Nashangaa wanaojiita wapenzi wasema kweli wanashindwaje Kutumia busara Kama hizi.
 

Kule bungeni sasa hivi ni kazi ya kuoneshana status za whatsup tu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Spika wa bunge nae ndio kinara wa pasia simu [emoji1]
 
Kanda ya ziwa haina uwanja wa michezowa kisasa kanda ya ziwa. Ajabu kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…