Wabunge wetu na CV zao

Komamanga

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2009
Posts
221
Reaction score
17
Mimi nafikiri kuna mambo mengine lazima tuangalie mzizi wake maana tunaweza tukawa tunaumiza vichwa kumbe sababu ya msingi hatuijadili.

Kiukweli kwa ninavyofahamu mimi ELIMU ndio ufunguo wa Maisha, Elimu ndio Kitovu cha Maendeleo, Elimu ndio chachu ya Maisha endelevu etc Kwa maana hiyo basi nafikiri sasa hivi ni wakati mzuri sana kujaribu kuangalia hadhi ya watu ambao tunawachagua na uwezo wao wa kuhoji mambo na masuala yote ya msingi ambayo yanaendeshwa na kupitishwa kwenye Bunge letu tukufu.

Nilikuwa najaribu kuhoji siku za karibuni kulikuwa na Wabunge wanatoa kauli tata na wengine wakitoa kauli ambazo zimefungua wananchi macho na zimekuwa chachu kwa mabadiliko japo kwa uduchu.

Nimejaribu kupitia tovuti ya Bunge na kugundua kwamba Kama Elimu ni kipimo cha maendeleo katika nchi basi Tanzania Kamweeeee na nathubutu kusema Kamweeeeeeeee maendeleo ambayo tunayaona kwa wenzetu ama kuyatamani kuwa nayo hayatatokea kama wataendelea kuwepo watu Vilaza ndio nasema Vilaza.

Kuna mtu katoka B.com akaruka mpk PhD, why??????Kwanini??????? Au ndio utaratibu wa elimu ya zamani, TUSIDANGANYANE BANAA

PLEASE, LET SAY NO TO THESE VILAZA HATUSAIDI

Please hembu tujaribu kuingia kwenye website ya Bunge tuone kuna wengine hata Elimu za msingi hazijawekwa sasa sijui wanahofia Uraia ama Aibu wanayoijua wao

Gonga hii mjionee Parliament of Tanzania

NOTE: HAYA NI MAONI YANGU BINAFSI
 
unakiwee weee!!!! elimu ni nzuri kwa wachache sio kwa tanzania yako
 
Ndiyo shule inaweza ikawa ni sababu, lakini si ya msingi sana kama ulivyosema hapa. Tuna wabunge wameenda shule vizuri lakini wanaongea na kutenda pumba. Cha maana ni uzalendo wa dhati.
 
First name Dr. Chrisant
Middle Name: Majiyatanga
Last Name: Mzindakaya
Date of Birth 31 December 1969
Bugerere - Uganda Secondary Education 1960 -1961 SECONDARY
Wakuu hiyo cv imekaaye website ya Tanzania parliament
 
Mhh nafikiri ni kukosa umakini tu kwa watendaji wetu,hilo ni kosa la kipuuzi sana
 
Mhh nafikiri ni kukosa umakini tu kwa watendaji wetu,hilo ni kosa la kipuuzi sana

Kinachopelekea kukosekana kwa umakini ni nini? Ndiyo hiyo shule finyu au anachozungumzia mwenzangu ... kukosa uzalendo?
 
No one pays attention to details, and no one cares after all. This is bongo bwana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…