Tatizo letu hatujui kama sisi ni wajamaaa, mabepari wa soko huria, wakomunisti wa ubepari beberu au tunaganga njaa tu bila mwelekeo wala dira kama alivyosema marehemu Kolimba.
Huwezi kutoa msimamo kama huu wa serikali au bunge linaloongozwa na CCM bila kujua CCM inafuata siasa gani.Tunafuata Azimio la Arusha, la Zanzibar au tamko la juzi la Kikwete ambalo nalo halijatafsiriwa likaeleweka.
Kuna watu wanaweza kusema wabunge wanahitajika katika mashirika ya umma ili wawe na uelewa wa kweli wa jinsi gani mambo yanaenda, na ndiyo sababu rais anateua wabunge wengi katika bodi za makampuni / mashirika ya umma.
Kuna wengine wanasema huu ni ukiritimba na kupeana ulaji tu, wabunge ni wanasiasa, tuwaache professionals wafanye kazi za professionals na wabunge wawe watunga sheria.
Vipi kuhusu walio wakurugenzi katika makampuni binafsi? Wao hawatakiwi kujiuzulu? Wao hawana issue ya accountability na conflict of interest?
Je, mbunge mwanasheria anayewawakilisha Barrick Gold Mines hawezi kuwa na conflict of interest na accountability issues katika kuuliza na kuchangia hoja zinazohusu biashara ya madini?
Mimi nilifikiri mashirika binafsi ni issue kubwa kuliko mashirika ya umma na kama kuna move ya wabunge kuacha ukurugenzi basi ingeanza huko.Kama bado wajamaa that is.
Kama mabepari of course you just let the market decide.