Wacha tuendelee kujidharau tu na kuwakweza wale

Wacha tuendelee kujidharau tu na kuwakweza wale

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Posts
11,478
Reaction score
3,659
Habari za asubuhi.
Mi huwa naweka mada hapo ili mradi ujumbe ufike. Kusomwa tu inatosha, hivyo wahusika wakiupata, wataufanyia kazi.

Sitakuwa specific ila nawaongelea hawa waswahili wanaotukuza race zingine. Mtu anaongea, tena in public ambapo ujumbe unafika mbali, kwamba katoto kazuri kama kasomali. Mara pua ya kisomali. Mara rangi ya mtume. Mara kaarabu flani. Mara ana asili ya kihindi, nk.

Hivi hao wahusika wanaotajwa wanawaonaje nyie waswahili? Ifike muda na wakati taasisi na mamlaka husika zitoe elimu ya utambuzi na ufahamu kuhusu kujikubali na kuwa wazalendo
 
Ni kweli mkuu, tunajidhalilisha sana watu Waafrika kwa kuonyesha uzuri ni waarabu, wasomali, Wabrazali na wazungu.
 
Kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza.
Unachotaka mkuu ni kufundishana kusema uongo kitu ambacho sio kizuri.
Waafrika ni wabaya? Hawako beatiful ukilinganisha na jamii nyingine?
 
Ila hao aliowataja jamaa wazuri Sana daaah, yaani kuanzia nywele, uzuri ndio usiseme
 
Hata hao na wenyewe wanapagawa na wa kwetu utasikia "black beauty"
Kifupi kila mtu anakiona cha mwenzio ndo kizuri kuliko cha kwake/kwao
 
Back
Top Bottom